WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI WATAKA SERIKALI KUTOWAONA WACHOCHEZI KATIKA JAMII.

Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Wat...








Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Serikali imeshauriwa kutoa ushirikiano kwa watetezi wa haki
za binadamu ili kurahisisha utendaji kazi wao badala ya kuwaona
watetezi hao kama wachochezi katika jamii na wakati mwingine kuwafungulia mashitaka.

Ushauri huo umetolewa hii leo Jijini Mwanza na Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, kwenye mafunzo ya siku tatu kwa
watetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Amesema katika baadhi ya maeneo kama Loliondo mkoani Arusha kwenye mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji, watetezi wa haki za binadamu wamechukuliwa kama wachochezi na kufunguliwa mashitaka jambo linalosababisha baadhi yao kushindwa kutekeleza majukumu yao na wengine kuacha kabisa shughuli za utetezi.

Akifungua Mafunzo hayo, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, amesema serikali itaendelea kuwaelimisha wachimbaji wadogo ili waifahamu vyema sheria ya madini namba 4 ya mwaka 2010
ili kupunguza migogoro iliyopo na kwamba imetenga zaidi ya hekta elfu 12 kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini.


Pia amesema serikali imetenga shilingi bilioni 6.6 kwa ajili
ya ruzuku kwa wachimbaji wadogo na kuwahimiza kujiunga kwenye vikundi ili wapatiwe ruzuku hiyo.


Baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha utendaji wao wa kazi jambo litakalowasaidia kutimiza vyema wajibu wao katika jamii bila kuonekana wachochezi huku pia wakiwa katika upande salama dhidi ya maisha yao.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza na wanahabari nje ya Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.

Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza na Wanahabari nje ya ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari.

Miongoni mwa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari.

Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari.

Washiriki wa Semina.

Mwonekano kwenye semina.

Picha ya pamoja.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI WATAKA SERIKALI KUTOWAONA WACHOCHEZI KATIKA JAMII.
WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI WATAKA SERIKALI KUTOWAONA WACHOCHEZI KATIKA JAMII.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjIL4U1eMWstlkGSfqfbUmdKXT90joGvl3nhU9U5i_HVUAlRIXiPcTUuA9whFeRx_zI4-EegXLgXjReZO0s4kh1vK8916r-tbgjMiWWKB3uDI2JOfzdoPmlgAqW5SA8hZ17EIxBhF9Rin4/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjIL4U1eMWstlkGSfqfbUmdKXT90joGvl3nhU9U5i_HVUAlRIXiPcTUuA9whFeRx_zI4-EegXLgXjReZO0s4kh1vK8916r-tbgjMiWWKB3uDI2JOfzdoPmlgAqW5SA8hZ17EIxBhF9Rin4/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/08/watetezi-wa-haki-za-binadamu-nchini.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/08/watetezi-wa-haki-za-binadamu-nchini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy