NITAHAMIA DODOMA SEPTEMBA MWAKA HUU - ASEMA WAZIRI MKUU MAJALIWA

*Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikap...




*Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.
 “Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo. 
Amesema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa ahadi alizotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

“Wananchi kazi mmeziona na sasa tunaenda kwenye utekelezaji. Ninatoa agizo kuwa mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja Dodoma. Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba, na utekelezaji wake nitausimamia kwa juhudi zote,” alisisitiza.
 Amewataka wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi. 
Wakati huo huo, mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika muda wa siku tatu amerudia kusisitiza nia ya Serikali kuhamia  Dodoma katika kipindi chake cha uongozi ili kutekeleza ndoto ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kutaka makao makuu ya nchi yawe Dodoma.
 Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma kwenye uwanja wa mashujaa huku akishangiliwa, Rais Magufuli amesema atahakikisha Dodoma inakuwa makao makuu ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobakia kwenye awamu ya kwnza ya uongozi wake.
 “Kama wabunge karibu 300 na mawaziri na manaibu wao ambao hawafiki 30 wanakaa hapa kwa miezi mitatu na maisha yanakwenda, kama makao makuu ya chama kinachotawala nchi yako hapa sioni sababu ni kwa nini Serikali ninayoiongoza iendelee kubakia Dar es Salaam,” amesema.
 Mara kwanza kutoa kauli hiyo, ilikuwa ni Jumamosi iliyopita, Julai 23, 2016 wakati akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkutano Mkuu maalum wa chama hicho.
 Rais Magufuli amesisitiza wananchi na wanasiasa kutunza amani na kudumisha amani iliyokuwepo nchini. Pia amewataka Watanzania wote kuendelea kuwaenzi mashujaa walioipigania nchi hii.
 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,    
DODOMA.
JUMATATU, JULAI 25, 2016.


Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.

Rais John Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi,Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016. Kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid na Naibu Spika wa Bunge, Dkt, Tulia Ackson.

Wananchi waliojitokeza kushiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma wakimsikiliza Rais John Maguguli wakati alipozungumza kwenye maadhimisho hayo mjini Julai 25, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma, Julai 25, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda  katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma, Julai 25, 2016. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, John Malecela (wa tatu kulia).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafari Mwanyembwa katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma, Julai 25, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma, Julai 25, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange na Kamishina Jenerali wa Magereza John Minja (kulia) katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa  mjini Dodoma, Julai 25, 2016.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa  mjini Dodoma , Julai 25, 2016. Watatu kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi , Jenerali Davis Mwamunyange na kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NITAHAMIA DODOMA SEPTEMBA MWAKA HUU - ASEMA WAZIRI MKUU MAJALIWA
NITAHAMIA DODOMA SEPTEMBA MWAKA HUU - ASEMA WAZIRI MKUU MAJALIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimVybtY2U4QaWXvhj_TK8m54AaQl9KfcB-QGYiNr6U79OuoLMcEXeBSZ7rCswdl0v2nwGN-E0ntwmyiRQBGTW0cCw1YQgH565lhhkoPGzm21K5cs0UZX11VSFoIxcIQLD7NFHKw_0ysYg/s640/IMGS7766.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimVybtY2U4QaWXvhj_TK8m54AaQl9KfcB-QGYiNr6U79OuoLMcEXeBSZ7rCswdl0v2nwGN-E0ntwmyiRQBGTW0cCw1YQgH565lhhkoPGzm21K5cs0UZX11VSFoIxcIQLD7NFHKw_0ysYg/s72-c/IMGS7766.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/07/nitahamia-dodoma-septemba-mwaka-huu.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/07/nitahamia-dodoma-septemba-mwaka-huu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy