BENKI YA TIB CORPORATE YATOA MSAADA WA MABATI 100 KWA SHULE ZA MKOA WA SONGWE.

Na Mwandishi Wetu Benki ya TIB Corporate leo imetoa msaada wa mabati   mia moja kwa mkoa wa Songwe ili kusaidia kukabiliana na u...





Na Mwandishi Wetu

Benki ya TIB Corporate leo imetoa msaada wa mabati  mia moja kwa mkoa wa Songwe ili kusaidia kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na  vyoo mkoani humo.
Mkoa wa Songwe, ambao ni miongoni mwa mikoa mipya, itatumia mabati hayo katika shughulli za ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wilaya za  Mbozi, Mamba, Ileje, Songwe na Tunduma.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya TIB Corporate, Bwana Frank Nyabundege alisema msaada huo umelenga kuonyesha nia na jitihada za benki yake katika kusaidia kukuza elimu na pia  kuunga mkono serikali katika jitihada zake za  kuboresha elimu nchini.
'Serikali pekee yake haiwezi kukuza sekta ya elimu hivyo basi ni muhimu tuisaidie serikali katika kuboresha sekta ya elimu kwa kuaanda mazingira mazuri kwa vijana wetu kujisomea’ alisema Nyabundege.
Akitoa shukrani zake kwa benki ya TIB Corporate, Mkuu wa mkoa wa Songwe Mheshimiwa Chiku Gallawa alisema mchango huo ni muhimu katika kukuza na kuboresha sekta ya elimu  ambayo ndio kichocheo cha ukuaji wa sekta ya uchumi na kijamii kwa taifa la kesho.
‘Tunaishukuru benki ya TIB Corporate kwa  jitihada zake za kushirikiana na serikali katika kukuza sekta ya elimu kwani hakuna taifa linaloweza kuendelea bila kuwa na raia wasomi ' alisema Mheshimiwa Gallawa.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akipokea msaada wa bando za bati kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Mkoa Mpya wa Songwe. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mbozi, Erik Ambakisye akifuatiwa na Mbunge jimbo la Vwawa Josephat Hasunga.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akipokea msaada wa bando za bati kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Bank, Bwana Frank Nyabundege (wa pili kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Mkoa Mpya wa Songwe. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mbozi, Erik Ambakisye akifuatiwa na Mbunge jimbo la Vwawa Josephat Hasunga.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BENKI YA TIB CORPORATE YATOA MSAADA WA MABATI 100 KWA SHULE ZA MKOA WA SONGWE.
BENKI YA TIB CORPORATE YATOA MSAADA WA MABATI 100 KWA SHULE ZA MKOA WA SONGWE.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjgHDRGGu9P-Hlsm6m2-jqQCIvJ77-MDe1UvgGUFzQpYaLFpPLsHAFSuY1PegoaVhaZU3kqEKoOlXg8ESDlc0_BcB3_dnFIfZda0uQvPWdmLEYIJLlYpFalYlH0AVrc9MTI4AmXRPDsDCg/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjgHDRGGu9P-Hlsm6m2-jqQCIvJ77-MDe1UvgGUFzQpYaLFpPLsHAFSuY1PegoaVhaZU3kqEKoOlXg8ESDlc0_BcB3_dnFIfZda0uQvPWdmLEYIJLlYpFalYlH0AVrc9MTI4AmXRPDsDCg/s72-c/1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/07/benki-ya-tib-corporate-yatoa-msaada-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/07/benki-ya-tib-corporate-yatoa-msaada-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy