Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo Leah Kihimbi akizindua mradi wa vyombo vya muz...
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo Leah Kihimbi akizindua mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) na
Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika katika Chuo cha Sanaa mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana.
Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika katika Chuo cha Sanaa mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana.
Msimamizi wa program wa Kituo cha Utamaduni na Maendeleo Denmark (CKU) hapa Nchini,Mandolin Kahindi akielezea utekelezaji
wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba), Michael Kadindena akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizaraya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo, Leah Kihimbi akipiga kinanda wakati wa
uzinduzi wa mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika katika Chuo cha sanaa Bagamoyo jana. Wanaoshudia katikati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba) Michael Kadindena kulia ni Mratibu wa Mradi huo, Melkiades Banyanka.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi akipuliza Tarumbeta ambacho ni moja ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Kituo cha utamaduni na maendeleo cha Denmark (CKU).
Meza kuu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (katikati) akiwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia burudani kutoka kwa wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati wa
uzinduzi wa mradi huo.
uzinduzi wa mradi huo.
Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakitoa burudani.
Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA),pamoja na wageni waalikwa wakishuudia kwa uzinduzi wa mradi huo.
Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), pamoja na wageni waalikwawakishuudia kwa uzinduzi wa mradi huo.
Picha ya pamoja.
..............................................................................................
KITUO cha Utamaduni na Maendeleo cha
Denmark (CKU), kimetoa msaada wa vifaa vya muziki katika Tasisi ya sanaa na
utamaduni Bagamoyo (TASUBA) vyenye thamani ya shilingi milioni 80 za
kitanzania.
Denmark (CKU), kimetoa msaada wa vifaa vya muziki katika Tasisi ya sanaa na
utamaduni Bagamoyo (TASUBA) vyenye thamani ya shilingi milioni 80 za
kitanzania.
Mbali na kununua vifaa vya
muziki,sehemu ya fedha hizo pia zitatumika katika matengenezo na usimamizi wa
vifaa hivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa mradi huo.
Akizungumza jana wilaya ya Bagamoyo
Mkoa wa Pwani Msimamizi wa program CKU hapa Nchini,Mandolin Kahindi anasema
kuwa ni moja fursa ya kuendeleza utamaduni na maendeleo ya kiuchumi.
Alisema kuwa msaada huo ni utekelezaji
wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa
ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
"Unajua mpango wa kuanza kutoa msaada Tasuba ulianza
mwaka 2014 baada ya CKU kukitembelea chuo hicho na kuelezwa kinakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa vifaa vya muziki vya kufundishia na
kujifunzia"alisema.
Alifafanua kuwa mpango huu wa kusaidia
uliazinduliwa rasmi juni mwaka jana ililenga kutengeneza fursa za kiuchumi
kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo watanzania watajipambanua kupitia
kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni na kujipatia kipato.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Sanaa Kutoka Wizara ya Habari ,utamaduni,sanaa,na michezo Leah Kihimbi
alisema kuwa amefurahi kupata msaada huo katika chuo cha sanaa lengo likiwa ni
kuendeleza vipaji hapa nchini.
"Katika chuo hiki ni kweli
kulikuwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia lakini sasa tumepokea msaada kutoka
katika Danish Centre for Culture and Development(CKU) kuweza kuwasaidia wanafunzi
katika chuo hiki.
Aliongeza na kusema kuwa ni jambo la
kuigwa kwa tasisi nyingine lengo ni kuweza kusaidia vyuo mbalimbali hapa
nchini.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
kuigwa kwa tasisi nyingine lengo ni kuweza kusaidia vyuo mbalimbali hapa
nchini.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
COMMENTS