Add caption Wafuasi wa Kasisi Felician Nkwera chini ya kituo cha Huduma za Maombezi wameandamana leo jijini Dar es ...
Add caption |
Wafuasi wa Kasisi Felician Nkwera chini ya kituo cha Huduma za Maombezi wameandamana leo jijini Dar es Salaam kumwomba mwenyezi Mungu aendeldee kuilinda amani ya nchi pamoja na kuombea amani iliyopo iendelee kudumu.
Pichani ni sehemu ya umati walioandamana kutoke eneo la Tazara mpaka Ubungo jirani na River Side wakifanya sala, mfululizo wakiwa wamebeba sanamu za bikira Maria, sakramenti ya ekaristi takatifu na kufukiza ubani kama ilivyo utamaduni wa kanisa katoliki lililomtenga kasisi huyo miaka mingi iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa uiliyotolewa na viongozi wa kituo hicho, haya ni matembezi ya sala ya tisa katika mfululizo wa matembezi ya sala ambayo huduma za maombezi zimekuwa zikifanywa jijini Dar es Salaam, Mbeya na Sumbawanga tangua ilipoanzishwa mwaka 1969.
'Huduma za maombezi ni utumemaalumwa sala za tiba: yaani uponyaji wa maradhi na kupunga pepo. Hauna ubaguzi kwa misingi yoyote na ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa Watanzania na ulimwengu mzima' Alisema Kasisi Nkwera.
COMMENTS