SIMBA SPORT CLUB YAWA YAKWANZA TENA, SAFARI HII NI KISASA ZAIDI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup, Iman Kajula akiongea  na waandishi wa habari wakati wa kuzindua mpango wa kuuza vifaa vya simb...







Simba SCAfisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup, Iman Kajula akiongea  na waandishi wa habari wakati wa kuzindua mpango wa kuuza vifaa vya simba kupitia duka la mtandao Dar es Salaam jana. Katikati ni Rais wa Simba, Evans Aveva na msemaji wa Simba Sport Club, Haji Manara.

Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Jumia wamezindua huduma ya kununua jezi za Simba 2015 – 2016 kupitia duka la mtandao la Jumia www.jumia.co.tz . Dhumuni la huduma hii ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya kuweza kununua jezi popote walipo Tanzania.
Kupitia mtandao imara na wenye uzoefu wa Jumia, klabu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake ya michezo nchi nzima. 

Mkataba huu utaongeza usambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu ya Simba. “Ukuaji kasi wa upatikanaji wa internet (mtandao) klabu ya Simba inafahamu umuhimu wa kuvifanya vifaa vyake vya michezo kuweza kupatikana kiurahisi kwa wateja wake, hivyo leo tunajivunia kuzindua huduma hii ya Jumia – Simba Online Shop kwa ajili ya kutumia mtandao wa Jumia kuwezesha wapenzi wa Simba popote walipo kuweza kununua mavazi na bidhaa az Simba kiurahisi na kwa bei nafuu”. Alisema Ras wa Simba Evans Aveva.
Maneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul aliongeza kwa kusema “uzinduzi wa jezi za mpira wa miguu siku zote ni tukio muhimu kwenye maisha ya klabu maarufu na inayopendwa kama Simba. Katika msimu wa 2015 – 2016 klabu ya Simba imeamua kuwa wabunifu kwa kutoa fursa kwa wapenzi wake kununua jezi za msimu 2015 – 2016 kupitia njia ya mtandao. Tunajivunia sana kwa Rais wa Simba Evans Aveva kutuchagua Jumia kwa kazi hii. Kupitia huu umoja wetu wa Simba na Jumia tumeamua kutoa ofa kwa wanachama na wapenzi wa Simba kuagiza jezi kuanzia Jumatatu tarehe 27 – 7 – 2015 mpaka Alhamisi 31 – 7 – 2015 kupitia www.jumia.co.tz kabla ya kuanza rasmi kwa mauzo ya kimtandao kupitia Jumia na kuanzwa kuuzwa rasmi kwa rejareja”.
“Tunawahamasisha wapenzi wa Simab popote walipo Tanzania kuagiza jezi kupitiawww.jumia.co.tz kuona urahisi katika kufanya manunuzi. Popote walipo wapenzi wa Simba wanaeza kuagiza jezi kupitia touti ya jumia na kuletewa mzigo wako mpka mlangoni. Jumia pia inatoa njia tofauti za ulipia kama ile kuweza kulipia pindi mzigo wakoutakapofika au kufanya malipo kwa njia za kipesa kupitia simu za mkononi. Kuanzia jumatatu 27 – 7 – 2015 wapenzi wa Simba watapatafursa ya kuagiza jezi kupitiawww.jumia.co.tz”. Aliongeza Maneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul.
Kuzungumzia mapinduzi haya makubwa katika usambazaji wa vifaa ya michezo ya klabu ya Simba Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAGgroup Limited Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara wa klabu ya Simba alisema “kwa mapinduzi haya makubwa yataiwezesha klabu ya Simba kuongezamapato yake pia kudhibiti bidhaa feki, kupitia Jumia Online Shops (duka la mtandao la Jumia) wapenzi wa Simba watanunua bidhaa za Simba kupitia washirika halali wa uuzaji wa bidhaa za Simba Tanzania.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SIMBA SPORT CLUB YAWA YAKWANZA TENA, SAFARI HII NI KISASA ZAIDI
SIMBA SPORT CLUB YAWA YAKWANZA TENA, SAFARI HII NI KISASA ZAIDI
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/07/Simba-SC.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/07/simba-sport-club-yawa-yakwanza-tena.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/07/simba-sport-club-yawa-yakwanza-tena.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy