MAUAJI YA KUTISHA YAFANYIKA KITUO CHA POLISI ASKARI WANNE NA RAIA WATATU WAPOTEZA MAISHA

HABARI za uhakika zilizotufikia leo asubuhi zimeeleza kuwa kituo cha polisi  Sitaki S hari Ukonga , jijini Dar es Salaam, kimevamiwa us...




HABARI za uhakika zilizotufikia leo asubuhi zimeeleza kuwa kituo cha polisi  Sitaki Shari Ukonga, jijini Dar es Salaam, kimevamiwa usiku wa saa 5 Julai 12, 2015 na watu wasiojulikana ambapo, askari polisi wanne na raia watatu wameuawa.




Pia silaha idadi isiyofahamika bado zimeporwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambapo kati ya hizo zimo SMG 15, SR 6 na risasi kadhaa.

Taarifa za majirani zinaeleza kuwa watu hao waliokuwa na silaha, walianza kupiga risasi ovyo kituoni hapo ambapo, askari wanne waliokuwa zamu, waliuawa. Taarifa za ndani kutoka Jeshi la polisi zinasema, raia watatu pia waliuawa kwenye shambulio hilo akiwemo mwendesha bodaboda mmoja aliyewaleta anayesadikiwa kushirikiana na wavamizi hao.

Raia wawili waliouwa walikuwa kituoni hapo kuwawekea dhamana ndugu zao waliokuwa mahabusu.

Taarifa zaidi zinasema, wavamizi hao hawakushughulika na mahabusu na baada ya kutekeleza unyama huo waliondoka na gari, walilokuja nalo hata, wavamizi hao walimuua kwa kumpiga risasi mwendesha bodaboda waliyekuwa wakishirikiana naye wakati wa  kuondoka kituoni hapo baada ya pikipiki yake kugoma kuwaka.

Majirani wanasema, milio ya risasi ilirindima kwenye eneo hilo na hali ilitulia majira ya saa 7 usiku.






Mwenyekiti wa Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam amabayee pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Saidi Meky Sadiki akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Eng. Raymond Mushi walitembelea kituo hicho kujionea yaliyotokea. 

Mojawapo ya pikipiki iliyokuwa ikitumiwa na mtuhumiwa aliyekuwa akishirikiana na wahalifu.


Msafara wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu ukiongozwa na gari la Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ukiwasili eneo la tukio.



Msafara wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu akikagua kituo hicho baada ya kuwasili kituoni hapo mchana huu.

Moja ya gari la Raia mwema aliyeuwawa wakati alipokwenda kituoni hapo kumepeleka mhalifu.






Msafara wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu uakiongea na waandishi wa habari kituoni hapo.

Watoto ndugu walioponea chupuchupu waliposhuhudia risasi zikirindima wakiwa wamehifadhiwa kituo hicho baada ya kuokotwa wakiwa wamepotea jana jioni. Watoto hao, (kutoka kulia), Richard, Rechol na Leah wametokea eneo la Ulongoni na wanasubiri wazazi ama ndugu wajitokeze kuwachukua. 
Mkazi wa jijini akipita jirani na moja ya nyumba ambapo ukuta wake ulipigwa risasi wakati majambazi hao wakisafisha njia baada ya kupora silaha nyingi kituoni hapo.









COMMENTS

BLOGGER: 1
Loading...
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAUAJI YA KUTISHA YAFANYIKA KITUO CHA POLISI ASKARI WANNE NA RAIA WATATU WAPOTEZA MAISHA
MAUAJI YA KUTISHA YAFANYIKA KITUO CHA POLISI ASKARI WANNE NA RAIA WATATU WAPOTEZA MAISHA
https://i.ytimg.com/vi/KbIppc-TmPo/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/KbIppc-TmPo/default.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/07/mauaji-ya-kutisha-yafanyika-kituo-cha.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/07/mauaji-ya-kutisha-yafanyika-kituo-cha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy