WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA WAJADILI MSUKOSUKO WA KISIASA BURUNDI, RAIS NKURUNZINZA ASHINDWA KUHUDHURIA.

Rais Jakaya Kikwete, akipozi kwa picha na mgeni wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumapili...






Rais Jakaya Kikwete, akipozi kwa picha na mgeni wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumapili Mei 31, 2015. Rais Kenyatta alikuwa nchini kuhudhuria mkutano wa kikanda kujadili mtikisiko wa kisiasa nchini Burundi, ambapo wananchi wamesalia mabarabarani nchini humo wakipinga mpango wa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunzinza kugombea urais kwa muhula wa tatu. Kiongozi huyo wa Burundi hakutokea kwenye mkutano huo.


Rais Kikwete, akisaliamiana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, wakati akiwasili kwenye mkutano huo.
Viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki akiwemo Raois wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, (Wakwanza kushoto), Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais Kikwete, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye kikao hicho


Rais Dkt.Jakaya Mrisho  Kikwete  akizungumza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Dkt.Nkosazana Dlamini-Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo ya amani ya Burundi


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma (kushoto), akisalimiana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, huku mwenyeji wa mkutano huo, Rais Jakaya Kikwete, akishuhudia. (Picha na Freddy Maro)


Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma (wa tatu kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa dharura wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam Mei 31, 2015. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Joyce Mapunjo na  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kulia) pia wakiimba wimbo wa Jumuiya hiyo.
Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.
Kundi la watu maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba  wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.
Juu na Chini ni Wajumbe mbalimbali wakifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi msaidizi katika ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Victoria Mwakasege nao wakifuatilia mkutano.
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini mkutano 
Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini nao wakifuatilia mkutano 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Assah Mwambene (katikati) pamoja na Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu, Macdonald Mwakasendile wakirekodi matukio.
Rais Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kumaliza mkutano.
Rais Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma kabla ya kuanza mkutano. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiongozana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta tayari kwenda kuanza mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Burundi .
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Vervaeke.

....Kuwasili kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alipowasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (NJIA).
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyetta akiwasili JNIAmara baada ya kuwasili nchini.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda mara baada ya kumpokea Rais huyo alipowasili katika JNIA.
Rais Museven akiwasili JNIA.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Balozi Radhia Msuya akisalimiana na Rais wa Afrika ya Kusini alipowasili JNIA.
Picha ya Pamoja baada ya mkutano wa wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. (Picha na Reginald Philip)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA WAJADILI MSUKOSUKO WA KISIASA BURUNDI, RAIS NKURUNZINZA ASHINDWA KUHUDHURIA.
WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA WAJADILI MSUKOSUKO WA KISIASA BURUNDI, RAIS NKURUNZINZA ASHINDWA KUHUDHURIA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXitzBc5iW6SRwAe1B-rWPeJNb6i4y5oKfV40Vw-Jgdv1f42AymonniT4T8kCRDMpmfG7EyBQZelHpRExDNTIEnWUN5Qrlrd9MBOJKWYMiio5moqdTyVhNOsFSLjpIGu55_4p4ySkwNGc/s640/D92A8983.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXitzBc5iW6SRwAe1B-rWPeJNb6i4y5oKfV40Vw-Jgdv1f42AymonniT4T8kCRDMpmfG7EyBQZelHpRExDNTIEnWUN5Qrlrd9MBOJKWYMiio5moqdTyVhNOsFSLjpIGu55_4p4ySkwNGc/s72-c/D92A8983.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/05/wakuu-wa-nchi-za-afrika-mashariki.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/05/wakuu-wa-nchi-za-afrika-mashariki.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy