Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya...
Mkurugenzi
Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja akizungumza na waandishi wa Habari
wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya Michezo kwa klabu ya mpira ya Lucenti,
itakayoshiriki michuano ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini, itakayofanyika
Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kushoto ni Meneja Fedha wa Benki hiyo, Patrick Kyamba
na Mwenyekiti wa Klabu ya Lucent, Yusuph Liambe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja,
Mwenyekiti wa Klabu ya Lucenti, Yusuph Liambe, Mkurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo
Margreth Kyarwenda wakiwa wameshikilia vifaa vya michezo vilivyotolewa na
Covenant Bank kwa timu hiyo itakayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za juu
kusini itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa.
************************************
Covenant
Bank yawaita TFF, yajitolea Kuwadhamini Twiga Stars.
Dar
es Salaam, 28 Aprili 2015 . . . Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank
Sabetha Mwambenja, amewaita viongozi wa Soka Nchini TFF, kwenda kujadili namna
ambavyo benki hiyo inaweza kuisaidia Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars
ambayo imefuzu kushiriki Michuano ya All African Games itakayo fanyika nchini
Congo mwezi Septemba.
Hayo
yametanabaishwa na Mkurugenzi huyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo
kwa timu ya Lucenti inayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za juu kusini
yatakayo fanyika Sumbawanga baada ya kufudhu michezo ya ligi dalaja la tatu
baada ya kuulizwa swali na waandishi waliotaka kujua ni namna gani benki hiyo
inaweza kuisaidia timu hiyo ya Taifa inayosuasua katika maandalizi.
“Hatuna
tatizo katika kuisaidia timu ya Taifa ya Wanawake tunaweza kuwasaidia kulingana
na Mahitaji yao, ni vyema viongozi wa soka (TFF) waje tukae tujadiliane ni
Namna gani tunaweza kuisaidia timu yetu ya taifa ili kuhakikisha inafanya
vizuri katika michuano hiyo inayokuja na mingine yote” alisema Mkurugenzi huyo.
Akikabidhi
vifaa hivyo kwa timu hiyo, kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika kwenye makao mkuu
ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi huyo, alisema wameamua kuvitoa
ikiwa ni sehemu ya kutambua ushirikiano wao na wananchi wa mkoa wa Ruvuma
hususani wilaya ya Namtumbo.
“Tumekuwa
tukishirikiana kwa masuala mengi ya kijamii na wanachi wa Namtumbo, tumesaidia
kujenga madarasa katika shule za msingi na maabara kwa shule za sekondari
wilayani humo kuwasadia ndugu zetu kukamilisha maagizo ya Rais yanayolenga
kuinua masomo ya sayansi nchini,” alisema.
“Kwa
kutambua umuhimu wa michezo, tumeona ni vyema tuchangie pia maendeleo ya soka
katika wilaya ya Namtumbo kwa kuipa vifaa vya michezo klabu ya Lusenti.”
Baada
ya kukabidhiwa vifaa hivyo vya Michezo, Yusuph Liambe, mwakilishi wa Mkuu wa
Wilaya Namtumbo, aliushukuru uongozi wa Benki ya Covenant kwa kutambua umuhimu
wa sekta ya michezo nchini na kuwapa vifaa hivyo ambayo alisema anaamini
vitaleta chachu ya timu ya Lusenti kufanya vyema katika mashindano ya soka
ngazi ya kanda yatakayoanza Mei 2, mwaka huu.
Katika
mashindano hayo yanayotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), klabu ya
Lusenti imepangwa Kanda ya Kusini pamoja na timu nyingine tisa kutoka mikoa ya
Njombe, Mbeya na wenyeji wa kanda hiyo mkoa wa Rukwa.
“Tunaamini
vifaa hivi vitawapa nguvu wachezaji wetu kujituma na kufanya vyema katika
michuano ya kanda, hivyo vipaji vyao kuonekana na kuchukuliwa na timu kubwa
ambazo zitawapa ajira,” alisema Liambe ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya
soka ya Lusenti.
COMMENTS