OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA PATO LA TAIFA KWA ROBO YA KWANZA YA MWAKA,JANUARY-MACHI 2014

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA PATO LA TAIFA KWA ROBO YA KWANZA YA MWAKA, JANUARY-MACHI 2014   Nembo ya Ofisi ya Taifa ya T...

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA PATO LA TAIFA KWA ROBO YA KWANZA YA MWAKA, JANUARY-MACHI 2014

 Nembo ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
 Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Morice Oyuke akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitoa taarifa ya pato la taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka kuanzia Januari na Machi 2014.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Oswald Ruboha, akizungumza katika mkutano huo.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi, Stephen Kirama akitoa ufafanuzi wa masuala ya uchumi katika mkutano huo. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
  Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Morrice Oyuke (wa tatu kushoto), akiwa  na wadau wa uchumi katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni  David Kwimbere kutoka ni Meneja Msaidizi wa Sera na Utafiti kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Oswald Ruboha, Mtakwimu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Royal Lyanga na Mtakwimu Mkuu wa NBS, Philemon Mahimbo.



 Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Morice Oyuke (katikati) akitoa ufafanuzi mbalimbali katika mkutano huo. Kushoto ni  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi, Stephen Kirama na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Oswald Ruboha.
 Wanahabari wakiwa katika mkutano huo wakipata taarifa taarifa hiyo



 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

SEKTA ZA MADINI ,UMEME NA KILIMO ZAKUZA PATO LA TAIFA.
 
Na. Aron Msigwa – MAELEZO
11/9/2014. Dar es salaam.

Sekta ya Kilimo,Uvuvi,  Viwanda , Nishati na Madini zimeelezwa kuwa miongoni mwa sekta muhimu zinazoongoza zaidi katika kuchangia kukua kwa pato la Taifa hadi asilimia 7.4 katika robo ya kwanza ya mwaka 2014.

Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya uzalishaji nchini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kutumia kanuni za kimataifa kukokotoa pato la Taifa zinaonyesha kuwa sekta hizo zimetoa mchango mkubwa wa kukua kwa pato la Taifa  kwa asilimia 7.4 kuanzia mwezi Januari hadi  Machi, 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.1 za mwaka 2013.

Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke akizungumzia ukuaji wa Pato la Taifa kwa bei ya Soko leo jijini Dar es salaam amesema kuwa Pato la Taifa katika robo ya mwaka 2014 kuanzia Januari hadi Machi limekua kwa asilimia 7.4 kutokana na kukua kwa sekta za Kilimo, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi, Umeme na  utoaji wa huduma.

Amesema sekta zilizofanya vizuri katika ukuaji huo ni pamoja na sekta ya uchimbaji wa Madini, mawe na kokoto ambayo imekua kwa asilimia 8.7 ikilinganishwa na asilimia 1.7 za mwaka uliopita kutokana na kukua kwa masoko ya uuzaji ya nje ya nchi.

Ameongeza kuwa sekta uzalishaji wa bidhaa za viwandani imekua kwa asilimia 8.5 kutoka 8.3 huku shughuli za utoaji wa huduma na uchumi zikiwemo za ukarabati wa magari, pikipiki na vifaa vingine vya majumbani zikikua kwa asilimia 8.0 kwa robo ya mwaka 2014.

Bw. Oyuke ameeleza kuwa shughuli za uchukuzi na mawasiliano zimefikia kasi ya ukuaji wa asilimia 16.5 katika kipindi hicho na kuongeza kuwa huduma za hoteli na migahawa zimefikia kasi ya ukuaji wa asilimia 3.0, huku shughuli za uendeshaji wa Serikali zikifikia asilimia 5.1, Elimu asilimia 5.2, huduma za Sfya na  shughuli nyingine zikikua kwa asilimia 4.5.

Aidha, amefafanua kuwa sekta ya umeme katika robo ya mwaka 2014 imekua kwa asilimia 12.6 ikilinganishwa na asilimia 6 ya mwaka uliopita kutokana na kupatikana kwa vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme hususan ugunduzi wa gesi nchini ambao umeondoa tatizo la utegemezi wa umeme wa maji katika kuzalisha umeme.

“Kwa kipindi kirefu sekta ya umeme imekuwa na mawimbi kwa kiasi kikubwa , umeme wetu umekuwa wa kutegemea maji ya mvua, baada ya juhudi za Serikali na kugundulika kwa nishati ya Gesi nchini na kupatikana chanzo mbadala cha nishati tatizo hili limeshghulikiwa sasa sekta hii imeimarika” Amesisitiza.

Amesema Tanzania sasa inafanya vizuri kiuchumi katika nchi za Afrika ya Mashariki kwa kuwa ya pili ikifuatiwa na Uganda, Rwanda na Burundi na kuongeza kuwa hali ya amani na utulivu iliyopo nchini inaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kukua zaidi kiuchumi.

Kwa upande wake mtaalam wa wa Uchumi kutoka Benki Kuu ya Taifa (BOT) Bw. Davidi Kwimbere akifafanua kuhusu hali iliyopo ya ukuaji wa uchumi amesema kuwa imechangiwa na kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji .

Amesema sekta ya Kilimo na uzalishaji wa mazao imekua kutokana na matumizi ya mbolea, zana bora za kilimo, mbegu bora, madawa na kufafanua kuwa endapo juhudi zaidi zitaendelea kufanywa na wananchi kwa kuingia katika shughuli mbalimbali za uzalishaji uchumi utaendendelea kuonekana kwa mtu mmoja mmoja.

Amefafanua kuwa maendeleo katika nchi yoyote  yanachukua muda na kutoa wito kwa nchi za Afrika kuendelea kujifunza  na kufafanua kuwa nchi zote zilizopiga hatua kimaendeleo mpaka kufikia asilimia 15 ikiwemo China iliwachukua miaka 20 kuondoa umasikini.

Amesema Tanzania inayo nafasi nzuri kukua kiuchumi kutokana na kuendelea kuimarika kwa miundombinu  na ukuaji wa sekta za ujenzi, Nishati, madini, Viwanda, umeme , kilimo na uvuvi hali inayochangia kuongezeka kwa uwekezaji.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA PATO LA TAIFA KWA ROBO YA KWANZA YA MWAKA,JANUARY-MACHI 2014
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA PATO LA TAIFA KWA ROBO YA KWANZA YA MWAKA,JANUARY-MACHI 2014
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiPz-NAWG63ZdHcP5Efk24N0cMQ2oDh2HrHHb1F268JQ7ppyEAsYAInH-HQtlmNWan889b7UmDcfQp8-4D91rV4FoWLGKM1kFnUU0spLQc9hCFg_gVogWoUwYgTjTATUGcIra2JrGyQ0c/s1600/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiPz-NAWG63ZdHcP5Efk24N0cMQ2oDh2HrHHb1F268JQ7ppyEAsYAInH-HQtlmNWan889b7UmDcfQp8-4D91rV4FoWLGKM1kFnUU0spLQc9hCFg_gVogWoUwYgTjTATUGcIra2JrGyQ0c/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2014/09/ofisi-ya-taifa-ya-takwimu-yatoa-taarifa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2014/09/ofisi-ya-taifa-ya-takwimu-yatoa-taarifa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy