MALASYA WAIFANYIA MAJARIBIO INJINI MPYA YA KWANZA YA TRENI ILIYOUNDWA KARAKANA KUU YA MOROGORO SAFARI YA KWANZA IMEANZIA DODOMA

MALASYA WAIFANYIA MAJARIBIO INJINI MPYA YA KWANZA YA TRENI ILIYOUNDWA KARAKANA KUU YA MOROGORO Meneja Mradi wa S.M.H RAIL kut...

MALASYA WAIFANYIA MAJARIBIO INJINI MPYA YA KWANZA YA TRENI ILIYOUNDWA KARAKANA KUU YA MOROGORO
Meneja Mradi wa S.M.H RAIL kutoka Malasya, V.Chalapathy pamoja na Meneja Ushauri wa Mradi wa Kampuni hiyo, Wenceslaus Kaijage wakiwa mbele ya injini mpya 88U01 kabla ya kuanza safari ya majaribio kwenda Mkoani Dodoma.

Baadhi ya mafundi na wananchi wakiangalia injini mpya ya Treni mara baada ya kuwasili stesheni ya Morogoro kutokea karakana ya TRL kabla ya kufanya safari ya majaribio kwenda Dodoma.

Hapa tayari treni ikiwa imefunga mabehewa ya mizigo kuelekea Dodoma.
 
Ikitoka kalakana kuelekea stesheni na behela la mafundi.

Ikitoka karakana na behewa la mafundi tayari kuelekea stesheni ili kubeba mahewa ya mizigo kwenda nayo Dodoma ikiwa safari ya majaribio. (PICHA/ MTANDA BLOG)


Na MTANDA BLOG, Morogoro.
KAMPUNI ya S.M.H.RAIL ya nchini Malasya leo imefanya safari ya majaribio ya injini mpya waliyoitengeneza kuanzia Stesheni ya Mjini Morogoro kwenda Mkoani Dodoma kwa mara ya Kwanza.
Majaribio ya injini hiyo namba 88U01 imeboreshwa kutoka kwenye ile ya awali iliyokua inafahamika kwa namba 8801 na kwa mujibu wa Meneja mradi wa Kampuni hiyo Bw V .Chalapathy injini hii ni ya kisasa zaidi na inatumia teknolojia ya kisasa ikiwa na nguvu ya HP 2300.
Meneja huyo akiwa na timu ya mafundi ambao wameondoka na treni hiyo amesema kwa majaribio injini hiyo itavuta tani 1125 za mzigo ingawa  uwezo halisi ni kuvuta tani 1300 kwa mwendo kasi wa Km 50 kwa saa kulingana na uwezo wa reli za hapa nchini na kwamba  kwa  Malasya injini hii inaweza kwenda umbali wa Km 130 kwa saa kwa kua miundo mbinu ya njia za reli ni mizuri.
Akizungumzia  katika stesheni ya mjini Morogoro jaribio la kwanza lilikua ni kutembeza injini yenyewe bila mzigo kwenda na kurudi Wilayani Kilosa na hili sasa ni jaribio la pili na baada ya hapo wataikabidhi injini hiyo kwa TRL kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo.
 Mshauri wa Mradi huo Wenceslaus Kaijage alisema injini hiyo ina mfumo wa udhibiti (Control unit) ambao kwanza unasaidia kuonyesha treni iko wapi na kwa wakati gani njia nzima inapokua safarini na kwamba mfumo huo unaruhusu kuisimamisha treni sehemu yoyote kwa kutokea stesheni au makao makuu kwa kutumia mfumo wa kompyuta.
Mmoja wa mafundi kutoka TRL ambao wako kwenye mradi huo wa kufufua injini hizo ameidokeza majira kua vifaa vipya vilivyokuja kutoka Malasya ni pamoja na injini yenyewe,Mashine ya mfumo wa upepo (Compressor) na Jenereta na kwamba vitu vyote vilivyobakia ikiwa ni pamoja na bodi na muundo wa injini hiyo vimefanyika katika karakana ya mjini Morogoro.
Stesheni Masta wa Mkoani Morogoro Flavian  Nyawale alisema kwa kua safari ni ya majaribio na bado injini hiyo bado iko mikononi mwa Kampuni hiyo wao jukumu lao ni kuwapatia mzigo kulingana na mahitaji ya majaribio yao ili kusoma tabia ya utendaji kazi wa injini hiyo kwenye hatua za awali.
“Kama injini haiwezi kufanya kazi kama inavyotakiwa huwezi kuipa namba kama hii ya 88U01 na badala yake inarudia ile ile 8801 hii herufi U maana yake ni Upgrading  yaani imeboreshwa kutoka kwenye ile ya awali” alisisitiza  Nyawale.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MALASYA WAIFANYIA MAJARIBIO INJINI MPYA YA KWANZA YA TRENI ILIYOUNDWA KARAKANA KUU YA MOROGORO SAFARI YA KWANZA IMEANZIA DODOMA
MALASYA WAIFANYIA MAJARIBIO INJINI MPYA YA KWANZA YA TRENI ILIYOUNDWA KARAKANA KUU YA MOROGORO SAFARI YA KWANZA IMEANZIA DODOMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpK6bMIYWvuKIPBsNXNzgjHBNYWOWFryDRkfQVvuKC-w4DUIjREsnK69hUygfr1qsgMgsgFnANWJSCgrK0lpCfU_SQHirgT68prerSR2y6eQyvz8oMgXsOlDOqSYeI15hTIUurbvc2eR3-/s1600/AZIZ+MSUYA+PIX+NO+3.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpK6bMIYWvuKIPBsNXNzgjHBNYWOWFryDRkfQVvuKC-w4DUIjREsnK69hUygfr1qsgMgsgFnANWJSCgrK0lpCfU_SQHirgT68prerSR2y6eQyvz8oMgXsOlDOqSYeI15hTIUurbvc2eR3-/s72-c/AZIZ+MSUYA+PIX+NO+3.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2014/01/malasya-waifanyia-majaribio-injini-mpya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2014/01/malasya-waifanyia-majaribio-injini-mpya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy