RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA ITIGI-MANYONI-CHAYA
HomeJamii

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA ITIGI-MANYONI-CHAYA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimb...



RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA ITIGI-MANYONI-CHAYA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipowasili Mkoani Singida eneo la Itigi ili kufungua Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa na Serikali kwa asilimia mia moja. Mheshimiwa Rais alikuwa akitokea kwenye ziara ya siku tatu Mkoni Tabora kupitia Singida akiwa njiani kuelekea  Dodoma  Julai 25,2017.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wa pili kushoto) na viongozi wengine wa mkoa wa Singida wakiondoa kitambaa kuashiria kufunguliwa rasmi kwa  barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida na Tabora Wakikata Utepe kama ishara ya kufunguliwa Rasmi kwa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiteta jambo na Mwakilishi wa Kampuni ya PowerChina International Group Limited nchini Bw. Wang Chao wakati wa Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwasalimia kwa kupunga mikono kwa wananchi wa Itigi na Manyoni walioshiriki na Kushuhudia Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Itigi na Manyoni walioshuhudia Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wananchi Kijiji Cha Tula Uyui Mkoani Tabora waliojitokeza Barabarani Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea kwenye ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo akiwa njiani katika moja ya mikutano ya barabarani kwa  waliojitokeza  Kumsalimia akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma akitokea kwenye ziara ya siku tatu Mkoni Tabora Julai 25,2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Itigi na Manyoni wakati wa Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja.
Wananchi wa Itigi na Manyoni wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatubia kwenye Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja. 
Picha zote na IKULU


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Itigi mara baada ya kuzungumza nao na kuzindua barabara Manyoni-Itigi-Chaya, ambapo pamoja na mambo mengine ameagiza ujenzi wa barabara ya Chaya-Nyaua yenye kilomita 85 na ujenzi uanze ndani ya siku 45 ili barabara hiyo ikamilike kwa kiwango cha lami.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na umati wa wakazi wa Itigi waliojitokeza kumlaki na kushuhudia uzinduzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, Rais Magufuli amewataka wana Itigi kutumia fursa ya kuwa jirani na Makao makuu ya nchi kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa huko Dodoma.
 Umati wa wakazi wa Itigi waliojitokeza kumlaki Rais Magufuli na kushuhudia uzinduzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, wakazi hao wamempongeza na kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwajengea barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa kuwaunganisha na mikoa ya Tabora na Kigoma.
 Sehemu ya barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya ambayo imezinduliwa leo na Rais Magufuli, Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 89.3 kwa kiwango cha lami imefungua fursa ya usafirishaji kwa urahisi kutoka kanda ya Kati yaani Singida na Dodoma Kuelekea mikoa ya Tabora na Kigoma hadi nchi za jirani za Burundi na Kongo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa akimkaribisha Rais Magufuli azungumze na wananchi wa Itigi, ambapo amesema barabara ya Manyoni Itigi Chaya imegharimu shilingi bilioni 114.692 na kiunganishi cha Mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma kuelekea Makao makuu ya Nchi yaani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi kwenye eneo la mkutano wa hadhara mara baada ya kuwasili eneo la Njiapanda Itigi, alipozungumza na wananchi wa eneo hilo na kuzindua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya.
 Umati wa wakazi wa Itigi waliojitokeza kumlaki Rais Magufuli na kushuhudia uzinduzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, wakazi hao wamempongeza na kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwajengea barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa kuwaunganisha na mikoa ya Tabora na Kigoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amkimsikiliza kwa makini Mhandisi wa TANROADS mkoa wa Singida Leonard Kapongo mapema leo. Katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Itigi, Rais Magufuli amemuagiza Meneja huyo na Wizara ya ujenzi kupitia upya gharama za ujenzi wa barabara ya Itigi Makongorosi yenye urefu wa kilomita 57 ambapo gharama za ujenzi wa barabara hiyo ni bilioni 104.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA ITIGI-MANYONI-CHAYA
RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA ITIGI-MANYONI-CHAYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg2Qv5hRQlBJVSz6619eajA2pABBH_iZWnb6taHJhdFoK_OXsX48Nta5lp_6KeX-B3JCYFXdDyJvDBMeVvbNdQXnfElZdT11BJAtYCWbxyK31AcsLtzfDEdJ0oIBHsfRoc1BzVYbATW1lc/s320/1+%25283%2529+%25282%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg2Qv5hRQlBJVSz6619eajA2pABBH_iZWnb6taHJhdFoK_OXsX48Nta5lp_6KeX-B3JCYFXdDyJvDBMeVvbNdQXnfElZdT11BJAtYCWbxyK31AcsLtzfDEdJ0oIBHsfRoc1BzVYbATW1lc/s72-c/1+%25283%2529+%25282%2529.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/07/rais-dkt-magufuli-afungua-barabara-ya_25.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/rais-dkt-magufuli-afungua-barabara-ya_25.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy