WAFANYABIASHARA MACHINGA COMPLEX WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
HomeJamii

WAFANYABIASHARA MACHINGA COMPLEX WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizungumza na wafanyabiashar...

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DK. HAMISI KIGWANGALLA ATEUA WAJUMBE WAPYA WA BODI YA MAMLAKA YA HIFADHI YA ENEO LA NGORONGORO
ELIMU YA AFYA YA UZAZI YASISITIZWA KUOKOA VIJANA KISIWANI PEMBA
RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex alipofanya ziara kwa ajili ya kusikiliza changamoto zao leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la Machinga Complex akielezea changamoto wanazokumbana nazo katika soko hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene (hayupo pichani) alipotembelea katika soko hilo leo Jijini Dar es Salaam. Waziri Simbachawene amefanya ziara katika Soko hilo hili kusikiliza changamoto kutoka kwa wafanyabiashara hao na kukagua utekelezaji wa agizo alilolitao wakati wa ziara yake ya kwanza sokoni hapo mapema mwaka jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene (wapili kutoka kushoto) akitembelea baadhi ya vizimba vya wafanyabiasha katika soko la wafanyabiashara wadogowadogo la Machinga Complex leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Meneja wa Soko hilo, na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando.

Na: Mpiga Picha Wetu.

………………

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dar es Salaam.

WAFANYABIASHARA ndogondogo katika Soko la Machinga Complex Jijini Dar es Salaam wameshauriwa kubadilika na kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria badala ya kufanya biashara zao kimazoea.

Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipofanyaa ziara ya kikazi katika Soko hilo ili kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo wafanyabiashara wa soko hilo.

“Nawapa pole sana ndugu zangu wafanyabiashara wa Machinga Complex mnaendesha biashara zenu bila kuzingatia sheria jambo linalo wagharimu hivi sasa katika biashara zenu leo nimekuja kuwarejesha kwenye mstari,” alisema Simbachawene.

Aidha Waziri Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuwachukulia hatua baadhi ya viongozi wa menejimenti ya Machinga Complex kwa kile kinachodaiwa utendaji wao mbovu na kujaza nadfasi zote zilizo wazi,

Wakati huohuo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuteua Wajumbe wa Bodi ya Machinga Complex ili kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa Soko hilo.

Pia Waziri Simbachawene ametoa wito kwa wafanyabiashara wote kulipa kodi zao kwa wakati huku hakitishia kuwaondoa katika vizimba (eneo la mraba la mauzo) wale wote watakao kaidi amri hiyo halali ya kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na mikataba yao.

Awali akimkaribisha Waziri Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa ujio wa Waziri huyo mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa imekuja wakati muafaka kwani ni takribani kipindi cha karibu mwaka mmoja tangu alipompa maagizo ya kushughulikia changamoto zinazokabili jengo la Machinga Complex kazi ambayo waliikamilisha na kukabidhi taarifa katika ofisi ya Waziri Simbachawene.

“Nidhahiri kuwa ziara yako Mhe. Waziri itatoa majawabu yatakayopelekea kutatua changamoto kadhaa zinazolikabili soko hili la Machinga Complex na ni imani yangu kwamba utatoa maagizo na kufanya maamuzi nasi hatuna budi ya kuyapokea na kutekeleza” alisisitiza Makonda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bibi. Sipora Liana amesema kuwa changamoto kubwa inayokabili Soko hilo ni pamoja na deni linalokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi bilioni 38 zianzodaiwa na Shirika la hifsdhi za Jamii (NSSF) ambao ndiyo waliojengwa majengo ya soko hilo linalomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine inayokabili Soko hilo ni kutokuwapo kwa chombo cha maamuzi (Bodi) ambayo kazi yake kubwa ingekuwa kushughulikia changamoto zote za mradi huo.

Soko la Machinga Complex limejengwa kwa lengo la kutatua changamoto ya ukosekanaji wa soko la uhakika kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika Jiji la Dar es Salaam ambapo ujenzi wake ulifanyika chini ya udhamini wa NSSF na kumilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam likiwa na uwezo wa kuchukua takribani wafanyabiashara 4206.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAFANYABIASHARA MACHINGA COMPLEX WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
WAFANYABIASHARA MACHINGA COMPLEX WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhd9NTL2mlTuZiMpJt0JiPyc4QJjMHcOHzk5nnXU8GJkEw6QjoorRTr6Gh6RM5u5_xb1B8rWQNoxKotSB3bERyB5L86k2ZPuX_XlWWmVM83jrBZy1CroWHTUDLDw5cK6LbvqwumBOczC70/s640/ETEQ.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhd9NTL2mlTuZiMpJt0JiPyc4QJjMHcOHzk5nnXU8GJkEw6QjoorRTr6Gh6RM5u5_xb1B8rWQNoxKotSB3bERyB5L86k2ZPuX_XlWWmVM83jrBZy1CroWHTUDLDw5cK6LbvqwumBOczC70/s72-c/ETEQ.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/wafanyabiashara-machinga-complex.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/wafanyabiashara-machinga-complex.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy