Wananchi wa Mtaa wa Mwambisi wakifua kwa kutumia maji ya mabondeni. Wakazi wa Mtaa wa Mwambisi Kata ya Kong...
Wananchi wa Mtaa wa Mwambisi wakifua kwa kutumia maji ya mabondeni.
Wakazi wa Mtaa wa Mwambisi Kata ya Kongowe iliyopo wilayani wakichota maji ya mabondeni kutokana na maji safi na salama katika kata hiyo kutoka mara moja kwa wiki na kusababisha kero na hofu kwa watumiaji wa maji hayo. Picha zote na Elisa Shunda
Mmiliki wa Blog ya Shunda Blog,Elisa Shunda, akichota maji kwa ajili ya matumizi ya kuoga
Wananchi wa mtaa huo wakielekea katika eneo la Bonde la Miti Mirefu kuchota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kama kufulia nguo,kupikia na kunywa jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa afya yao.
NA: ELISA SHUNDA,KIBAHA
Serikali
imeombwa kuingilia kati suala la ukosefu wa upatikanaji wa maji safi
katika kata ya Kongowe eneo la Mwambisi ambalo maji yamekuwa yakitoka
mara moja kwa wiki na kusababisha wananchi kutumia maji ya mabondeni
yasiyo salama kwa matumizi ya binadamu.
Wakizungumza
na Raia Tanzania,jana wakazi wa maeneo mbalimbali wa kata hiyo walisema
kuwa kutokana na kutopatikana kwa maji safi na salama kwa wakati
timilifu imepelekea watoto wananchi kuwa na mashaka na afya zao kwa
kuhofia kupata magonjwa mbalimbali kama kuhara,kuumwa matumbo na
kichocho.
Akichangia
hoja hiyo mkazi wa mtaa wa Mwambisi,Maria Nicoulas alisema kuwa
kutokupatikana kwa maji safi katika eneo la mwambisi ni kero kubwa sana
kwa akina mama ambao muda mwingi wanautumia kusubiri maji mabondeni na
pia maji yenyewe siyo salama kwa matumizi ya nyumbani lakini pia inaweza
ikagombanisha familia kati ya baba na mama kwa kuingiza hisia tofauti
kwa kuwa unaweza ukakaa kusubiri uchote maji hata masaa matatu.
“Sisi
akina mama tunapata shida sana kupata maji kwa kuwa hata sehemu
tunapoenda kuchota maji ni mbali na nyumbani na pia maji yenyewe huko
kwenye mabonde ya mpunga ni mbali inachukua muda mwingi hadi kuludi
nyumbani kwa hali kama hii inaweza kusababisha ugomvi kati ya baba na
mama kwa kuingiza suala la wivu wa kimapenzi kumbe masikini ni kutokana
na umbali wa sehemu tunapochota maji na foleni iliyopo hivyo tunaiomba
serikali iangalie kuhusu tatizo hili”Alisema Maria
Mkazi
wa Bamba, Juma Abdul,alisema kuwa kutokana kukatika mara kwa mara kwa
maji katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo imekuwa ni kero na usumbufu
kwa wananchi ambapo huwaletea kutumia fedha nyingine ya ziada kununua
maji safi wakati mabomba yapo lakini hayatoi maji.
Aidha
wananchi hao wananchi hao wameiomba serikali kutoa msaada wa hali na
mali kuhakikisha huduma hiyo muhimu inarejea kama hapo awali ili kuondoa
uwezekano wa kutokea milipuko ya magonjwa ya matumbo na kichocho.
Akichangia
kuhusu kero hiyo Aliyekuwa mgombea Udiwani wa kata hiyo kupitia Chama
cha Wananchi (Cuf), Mathas Kambi alisema kuwa suala la maji safi na
salama kwenye kata ya kongowe ni tatizo sugu sana, linatokana na sababu
kuu zifuatazo kwanza viongozi wa kata pamoja na viongozi wa serikali za
mitaa kutotambua ufuatiliaji wa kero hiyo, pili dawasco wenyewe pia
hawako sawa kwenye huduma zao, kwa maana miundombinu yao kwenye
usambazaji haipo sawa.
“bomba
kubwa linaweza kuharibika visiga wiki nzima watu wa kongowe tunaweza
kukosa maji kutokana na tatizo hili afadhali ya mwambisi na Bamba maeneo
ya kwamwami upande wa kulia kama unaenda mlandizi kule hawajui maji
tokea kongowe imefahamika eneo la bamba upande wa kushoto kuna watu
wamechangishwa pesa na mwenyekiti wao Mavala mamilion ya pesa mpaka leo
maji hakuna ni utapeli mtupu , miembe saba B toka imezaliwa mpaka leo
hawajui lini watapata maji safi na salama ,huko mwambisi ndiko tatizo
kama linavyojionyesha”Alisema Kambi
Akizungumza
kuhusu suala hilo Diwani wa Kata ya Kongowe, Iddi Kanyalu alisema kuwa
tatizo hilo limefika ofisini kwake na kusema kuna shida ya kukatika kwa
maji sana katika eneo la Mwambisi na Vikunai na ameshalipeleka katika
ofisi za Shirika la majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASCO)
wilaya ya Kibaha alisema uongozi wa shirika hilo wamemuambia kuwa
tatizo kubwa ni baadhi ya wananchi wanajiunganishia mabomba kiholela na
muda si mrefu wataanza kufanya oparesheni katika makazi ya watu.
“Nimepata
taarifa za kuwepo kwa shida ya maji katika maeneo mbalimbali ya kata
yangu ya Kongowe nimefikisha kwa uongozi wa Dawasco ambapo wameniambia
kutokea kwa hali ya kukatika maji sababu kubwa ni baadhi ya wananchi
ambao si waaminifu wamejiunganishia mabomba kinyume na sheria hali
inayosababisha ukiosefu wa maji na pia uongozi umeniambia kuanzia wiki
hii wanaanza oparesheni ya kupitia katika makazi ya watu ili kubaini
watu waliojiunganishia maji kiholela”Alisema Kanyalu
COMMENTS