RAIS MAGUFULI AMPOKEA RAIS MUSEVENI JIJINI ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakiongea...







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakiongea na wanahabari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
 Rais Museveni akizungumza wakati yeye na mwenyeji wake. Rais Magufuli, walipozungumza na waandishi wa habari February 1, 2016.
Rais Museveni akiwa na mwenyeji wake Rais Magufuli Ikulu ndogo jijini Arusha.


 
************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, amekutana na kufanya Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Tanga nchini Tanzania hadi nchini Uganda.

Rais Museveni amemtembelea Rais Magufuli katika Ikulu ndogo ya Arusha jioni mara baada ya kuwasili hapa nchini akitokea nchini Uganda, ambapo hapo kesho atahudhuria Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, utakaofanyika katika Hoteli ya Ngurudoto jijini Arusha.

Akizungumza baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo ya faragha, Rais Magufuli amesema wamekubaliana kutekeleza mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanga hadi Uganda, kwa manufaa ya nchi zote mbili na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Amesema bomba hilo litakuwa na urefu wa Kilometa 1,120 na kwamba mradi huo utazalisha ajira za watu zaidi ya 15,000.

Rais Magufuli ameongeza kuwa pamoja na kujengwa kwa bomba la mafuta, pia wamezungumzia kuongeza biashara ndani ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, kujenga viwanda na kuzalisha ajira zaidi kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji mali.

Aidha, Rais Magufuli amesema katika Mkutano huu nchi wanachama watajadili maombi ya nchi ya Sudan Kusini kupata uanachama ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amebainisha kuwa, kwa Sudan Kusini kuwa mwanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki, itakuwa na uwezo wa kufanya biashara katika eneo lenye takribani watu milioni 150 na hivyo kupata manufaa makubwa zaidi.



Kwa upande wake Rais Yoweri Kaguta Museven pamoja na kuunga mkono yaliyosemwa na Rais Magufuli amempongeza kwa kasi yake nzuri aliyoanza nayo katika uongozi, na amesema ni matumaini yake kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, sasa zitakuwa katika nafasi nzuri ya kwenda kwa kasi ya Rais Magufuli katika maendeleo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI AMPOKEA RAIS MUSEVENI JIJINI ARUSHA
RAIS MAGUFULI AMPOKEA RAIS MUSEVENI JIJINI ARUSHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitCpOQvCYTHRdMa3g-bM9ncBlq5PXug4Cv7MABmgvUIXe6N3QDxOmVe9Juq_1I62GRl3VywBWLhGg706Mhqr_eTdlio5g3QZK9tNQjlUa04EPpvLrkNBtpASzM9aWgyj4h-jGLXw2lzjsU/s640/mu3.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitCpOQvCYTHRdMa3g-bM9ncBlq5PXug4Cv7MABmgvUIXe6N3QDxOmVe9Juq_1I62GRl3VywBWLhGg706Mhqr_eTdlio5g3QZK9tNQjlUa04EPpvLrkNBtpASzM9aWgyj4h-jGLXw2lzjsU/s72-c/mu3.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/03/rais-magufuli-ampokea-rais-museveni.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/03/rais-magufuli-ampokea-rais-museveni.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy