Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Nchini (NEC), Ramadhan Kailima akiongoza kikao maalum cha menejimenti ya Tume wakijadili vipaumbele ...
Na Mwandishi-NEC
Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza kupitia vipaumbele kwa
ajili ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017.
Katika kikao chake cha Menejimenti kilichofanyika Januari 11, 2016,
baadhi ya vipaumbele vinavyoendelea kujadiliwa ni uhuishaji wa Sheria mbalimbali
zinazosimamia masuala ya uchaguzi, Elimu ya Mpiga Kura, na ujenzi wa ofisi ya Tume.
Vipaumbele vingine vinavyojadiliwa ni pamoja na miongozo na mifumo ya ufuatiliaji
na tathmini, mifumo ya uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura na mifumo
ya uendeshaji wa Uchaguzi.
Tume imeanza mandalizi haya ili kujipanga vema ili mwongozo wa Bajeti utakapotoka,
Menejimenti ya NEC iwe imekamilisha hatua zote za awali na kusubiri kuwasilisha
katika ngazi husika.
Huu ni utaratibu mpya ulioanzishwa na Tume ya Uchaguzi ili kuhakikisha masuala
yote muhimu yanakuwepo katika uandaaji wa Bajeti ya mwaka
wa fedha wa 2016/2017.
Vikao hivi vya Menejimenti ya Tume ni vikao vya kawaida vinavyofanyika kila
Jumatatu kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa kila Idara na
kujipanga kwa utekelezaji wa wiki inayoanza.
SMS
+255(0)772 55 55 53
LISTEN LIVE
http://myradiostream.com/ FocusRadioTz
Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Tanzania
FACEBOOKLISTEN LIVE
http://myradiostream.com/
Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Tanzania
http://bitly.com/1zIiIkq
http://bit.ly/1678Vq2
WEBSITE
http://www.nec.go.tz
COMMENTS