BENKI YA CRDB YAADHIMISHA SIKU YA WATEJA

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kulia) akizun...


Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kulia) akizungumza na  wateja waliofika katika tawi la Holland House jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ,Esther Kitoka (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wateja waliofika katika tawi la Tabata jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB ambapo viongozi wa benki hiyo wamekuwa wakitoa huduma za kibenki katika matawi mbalimbali ya benki hiyo. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (wa pili kulia) akisalimiana na wateja waliofika katika tawi la PPF Tower jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB. Kulia ni Mkurugenzi wa tawi la PPF Tower, Can Meseyeck. 
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi Tabata, Hawa Sasya akisalimiana na watoto wa shule ya African Nursery & Primary School ya Tabata jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB iliyoanza Oktoba 6.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto), Mkurugenzi wa tawi la Holland House, wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Sport FM cha Dodoma, Abdallah Majura (kulia) akipongezwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakati maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea tawi la Azikiwe Premier jijini Dar es Salaam.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) akikata keki na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula wakati maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula akimlisha keki Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyoSaugata Bandyadhiyay ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyoSaugata Bandyadhiyay akimlisha keki  Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDBSaugata Bandyadhiyay (wa nne kutoka kulia), Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo pamoja na maofisa wa CRDB.

Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa wamepozi kwa picha.
Picha ya pamoja
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma katika tawi la Holland House.

Mkurugenzi Mkuu wa Msae Investment, Wilbard Mtenga akipokea keki kutoka kwa  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDBSaugata Bandyadhiyay wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wateja wa benki ya CRDB. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya CRDB inaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kusikiliza matatizo yanayowakabili wateja wa benki hiyo.
Akizungumza alipotembelea matawi ya Holland, Premier na PPF Tower jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Saugata Bandyadhiyay, alisema kuwa wanatumia wiki hiyo katika kusikiliza matatizo ya wateja ili kuboresha huduma.
Bandyadhiyay alisema pia watasikiliza kero za wateja pamoja na kupata maoni juu ya huduma inayotolewa na benki hiyo ikiwa ni pamoja na kuyatatua.
Alisema CRDB itahakikisha inatoa huduma kwa usikivu, uwajibikaji, nia, ubunifu ushirikiano na ufanisi ili kuongeza tija kwa wateja wanaowahudumia.

Naye Meneja wa akaunti tawi la Premier, Nellie Mwambapa, aliwataka wateja kuhakikisha wanafika na kuandika maoni yao ikiwa ni pamoja na kuleza mapungufu ili CRDB iendelee kutoa huduma bora.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BENKI YA CRDB YAADHIMISHA SIKU YA WATEJA
BENKI YA CRDB YAADHIMISHA SIKU YA WATEJA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgyAutPrLA_eXzgH8YiZklAAi_Mf9xYU_OWZ9rSupARq9V1cV6qhfNzL04efkt9SsDRwpneKkaPHG-F_w_Cc-Tp7-ovsBBHegsnZmseRB3apZVB9mxjAE3JIqjSCIJG9G0wqgLnwk_7B_Y/s1600/Pix-1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgyAutPrLA_eXzgH8YiZklAAi_Mf9xYU_OWZ9rSupARq9V1cV6qhfNzL04efkt9SsDRwpneKkaPHG-F_w_Cc-Tp7-ovsBBHegsnZmseRB3apZVB9mxjAE3JIqjSCIJG9G0wqgLnwk_7B_Y/s72-c/Pix-1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2014/10/benki-ya-crdb-yaadhimisha-siku-ya-wateja.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2014/10/benki-ya-crdb-yaadhimisha-siku-ya-wateja.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy