Meneja Mawasiliano na Matukio wa Vodacom Tanzania, Christina Chacha (wa pili kushoto) akifurahia jambo na mtoto Anna Rajabu ana...
Watoto wenye maradhi ya saratani wanufaika na lishe bora
Watoto
wanaosumbuliwa na maradhi ya saratani ambao wanaendelea na matibabu
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamepatiwa msaada wa lishe ili
kupunguza tatizo la kupata lishe duni ambalo
limekuwa tatizo sugu linalowaathiri watoto wengi nchini.
Ukosefu
wa chakula bora chenye virutubishi vinavyotakiwa mwilini ni moja ya
tatizo ambalo limekuwa likipelekea watoto wengi kunyemelewa na magonjwa
mbalimbali kutokana na kupunguza kinga
ya mwili na wale wenye magonjwa kuchelewa kupona kutokana na lishe
duni.
Msaada
huo wa lishe umetolewa mwishoni mwa wiki katika wodi ya watoto ya
hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia
Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha
na kuwahudumia watoto wenye maradhi ya Saratani linalojulikana kama
Tumaini la Maisha.
Akiongea
wakati wa kupokea msaada huo Mratibu wa mradi huo Dk.Jane Kaijage
alishukuru msaada huo kutoka Vodacom Foundation kwa watoto utakaowafikia
na kuwanufaisha walengwa kupitia taasisi
ya Tumaini la Maisha.
Alisema
kuna idadi kubwa ya watoto zaidi ya 300 wanaolazwa hospitalini hapo
wakiwa wanakabiliwa na saratani ya aina mbalimbali na kutokana na umri
wao lishe bora ni muhimu kwao sambamba
na matibabu wanayoendelea kuyapata ili wapone haraka.
Kwa
upande wake Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza alisema kuwa
siku zote taasisi hiyo itakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za
serikali katika kusaidia jamii hususani
katika nyanja za Afya na Elimu.
“Afya
ni moja ya suala ambalo tunalipa kipaumbele na ndio maana tumekuwa
tukivalia njuga kutokomeza magonjwa mbalimbali mojawapo ikiwa ugonjwa
huu wa saratani ambao siku hadi siku umekuwa
ukiongezeka na kusababisha vifo vya watu wengi”Alisema.
Alisema
Vodacom Foundation imetoa kiasi cha shilingi milioni 26 kupitia taasisi
ya Tumaini la Maisha ili kuwawezesha watoto hawa kupatiwa chakula bora
na matunda kwa ajili ya kuwajengea
afya bora hususani katika kipindi hiki kigumu wanachoendelea kupata
matibabu na aliwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia wenye matatizo
mbalimbali kwenye jamii.
Mmoja
wa wazazi ambaye mtoto wake anaendelea na matibabu ya Saratani Jane
Paulo kutoka mkoani Kigoma akiongea kwa niaba ya wenzake alishukuru
Vodacom Fondation kwa msaada huu muhimu wa
lishe kwa watoto wao katika kipindi hiki kigumu ambacho wanaendelea
kupata matibabu.
Alisema
kwa msaada huo taasisi hiyo imethibitisha usemi wa akufaaye kwa dhiki
ndiye rafiki kwa kuwa umetolewa katuka muda mwafaka ambao watoto
wanahitaji kupata lishe bora wakati huo wazazi
wengi wakiwa wanakabiliwa na changamoto ya kutomudu kununua vyakula
muhimu kutokana na kukabiliwa na ugumu wa maisha ambao unasababishwa na
kutumia muda wao mwingi kuuguza watoto badala ya kujishughulisha na kazi
za kuwaingizia vipato.
Children living with cancer get nutrition support
Children
who are suffering from cancer who are undergoing treatment at Muhimbili
National Hospital have been provided nutritional support
from Vodacom Foundation to alleviate the problem of poor nutrition
which has been a chronic problem affect many children in the country.
Foundation has provided a grant of Tshs 27 million
to
this program that will provide these little patients with adequate
nutrition which implement through Tumaini La Maisha, a local Non
Government Organization.
Speaking
at an event at Muhimbili National Hospital to mark the offering of the
grant, Tumaini la Maisha’s Project Manager,Dr.Jane Kaijage
revealed that so far the program expect to benefit more than 300
children each year for various type of Cancer admitted at the hospital .
“During
cancer treatment, poor nutrition is a leading complication to healing.
Chemotherapy in itself leaves patients
with weakened immune systems and difficulty tolerating much food. Poor
nutrition might also be a cause to the initial cancer, since a lack of
essential vitamins and minerals can reduce immunity for the body to
fight off cancer cells. Eating the right types
of food before, during and after treatment can help the child feel
better and stay stronger”
Dr.Kaijage said
in order to improve the children’s health and progress in treatment,
the children will be fed whole, plant-based foods often in the form of
smoothies and juices that can be easily digested.
For his part, the Head of Vodacom Foundation, Mr. Renatus Rwehikiza noted that the Foundation’s grant of Tshs 27 million
through the institution of Hope of Life in order to enable these
children to be provided with good diet to them for building healthy,
especially in this difficult period progresses to the treatment and
urged other stakeholders to emerge to help with various
problems in society
“Vodacom
Foundation will always forefront to support government efforts in
helping the community, especially in the fields of health and
education and urged other stakeholders to emerge to help with various
problems in society.
One
of the parents whose child is undergoing treatment for cancer Regina
Paulo from Kibondo in Kigoma region speaking on behalf of his colleagues
thanked Vodacom Foundation for this important nutrition support for
their children during this difficult time that they continue to get
treatment.
Recent
studies have shown that survival rates of children with cancer are
significantly improved with a diet plentiful in
fruits, vegetables and whole grains. The nutrition program will
improve digestive health, prevent malnutrition and provide dietary
supplements in the hope of keeping the children strong, nourished and
able to heal. The Vodacom Foundation’s charity is playing
a valuable role in keeping this program going
COMMENTS