MAGAZETI YA TSN YAWA YA KWANZA KUPATA LESENI ZA BAADA YA AGIZO LA SERIKALI LA AGOSTI.

Serikali Yaanza kukabidhi Leseni kwa Kwa Machapisho, Jarida la Nchi Yetu. Na Neema Mathias na Paschal Dotto- MAELEZO. Serikali kupi...





Serikali Yaanza kukabidhi Leseni kwa Kwa Machapisho, Jarida la Nchi Yetu.


Na Neema Mathias na Paschal Dotto- MAELEZO.

Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) imeanza rasmi utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari kwa kutoa leseni kwa vyombo vya machapisho yakiwemo Magazeti na Majarida.


Akizungumza katika makabidhiano ya leseni hizo Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema utoaji wa leseni ni utekelezaji wa agizo rasmi lililotolewa Agosti 23, 2017 lililowataka wamiliki wote wa machapisho kujisajili upya na kupewa leseni kwa lengo la kuifanya tasnia ya Habari kuwa taaluma rasmi kama zingine.

“Leseni hizo zimeanza kutolewa rasmi Agosti 23 na zoezi hilo litaendelea hadi Oktoba 15, 2017 na baada ya hapo wale amabo watachapisha magazeti na majarida bila kuzingatia Sheria hiyo watakuwa wametenda kosa la jinai”, alisema Dkt. Abasi.

Katika zoezi hilo Dkt. Abbasi alitoa leseni kwa vyombo vinne ambavyo ni Jarida la Nchi Yetu linalomilikiwa na Idara ya Habari MAELEZO, gazeti la Daily News, Habari Leo pamoja na Spoti Leo ambayo ni magazeti ya Serikali.

Dkt. Abbasi ametoa wito kwa vyombo vingine vya habari ambavyo bado
havijaanza taratibu za upataji wa leseni visisubiri hadi dakika za mwisho za mchakato huo ili kuepuka msongamano na usumbufu usio wa lazima.

“Nitumie fursa hii kuwaalika ambao hawajapata leseni wafanye haraka, Tanzania Standard Newspaper (TSN) walitimiza masharti ndani ya siku tatu ndio maana leo wamepata leseni hizo, hakuna urasimu wala nia mbaya ya kufungia baadhi ya machapisho kama wengi wanavyodai bali ni katika kutekeleza matakwa ya Sheria”, alisisitiza Dkt. Abbasi.

Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa TSN Dkt. Jim Yonazi ameviasa Vyombo vingine vya Habari kutekeleza agizo hilo ili kupata uhuru mpana katika uwajibikaji pamoja na kuwa mfano wa kutii Sheria bila shuruti ili taaluma ya habari iendelee kuheshimika kwa jamii.

“Ukifanya kazi kihalali unakuwa na uhuru wa kufanya kazi vizuri, ubunifu unaongezeka na unafanya biashara bila wasiwasi”, alisisitiza Dkt.Yonazi.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la Daily News mwakilishi wa gazeti hilo Bi. Pudenciana Temba. Idara ya Habari imetoa imetoa leseni nne kwa ambapo leseni namba moja imetolewa kwa Jarida la Nchi Yetu linalotolewa na Idara hiyo, namba mbili imetolewa kwa HabariLeo, namba tatu Dailynews na nne imetolewa kwa Spotileo.Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Usajili Bw. Patrick Kipangula.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la HabariLeo mwakilishi wa gazeti hilo mhariri wa gazeti hilo Bw. Amir Mhando leo Jijini Dar es Salaam. Leseni hiyo imetolewa kufuatia kuanza kwa matumizi ya sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimpongeza Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayomiliki magazeti ya Daily News, Sunday News, HabariLeo na SpotiLeo, Dkt. Jim Yonazi kwa Kampuni yake kuzingatia matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kwa kujisajili upya na kupatiwa leseni.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa magazeti ya HabariLeo, Sunday News, Daily News, SpotiLeo yanayomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na uongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mara baada ya kukabidhiwa Leseni za usajili wa magazeti hayo Agosti 30 2017, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija - MAELEZO)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAGAZETI YA TSN YAWA YA KWANZA KUPATA LESENI ZA BAADA YA AGIZO LA SERIKALI LA AGOSTI.
MAGAZETI YA TSN YAWA YA KWANZA KUPATA LESENI ZA BAADA YA AGIZO LA SERIKALI LA AGOSTI.
https://i.ytimg.com/vi/zGtT0vnKmNw/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/zGtT0vnKmNw/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/magazeti-ya-tsn-yawa-ya-kwanza-kupata.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/magazeti-ya-tsn-yawa-ya-kwanza-kupata.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy