Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa mkutano wa wadau na wataalam wa e...
Na. Aron
Msigwa.
26/3/2015. Dar es salaam.
Chuo cha Elimu ya
Biashara Kampasi ya Dar Es salaam (CBE) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa
elimu nchini kiko katika hatua za mwisho za kukamilisha Mtaala wa kufundishia Walimu
wa masomo ya biashara kwa ngazi ya shahada utakaoanza kutumika katika mwaka
masomo utakaoanzia mwezi Septemba 2015.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau na
wataalam wa elimu kutoka Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara
wa shule za Sekondari na vyuo na wadau
mbalimbali wa Elimu leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel
Mjema amesema chuo chake kimeamua kuanzisha programu hiyo ili kuziba pengo la
uhaba wa walimu wa kufundisha masomo ya Biashara wenye taaluma ya ualimu.
Amesema chuo hicho kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali kimefikia uamuzi huo kufuatia utafiti uliofanywa na jopo la wataalamu wa
maandalizi ya Mtaala huo kuanzia mwaka
2012 uliobaini uwepo wa kiwango kikubwa
cha uhitaji wa waataalam wa kufundisha masomo ya biashara wenye taaluma ya
ualimu.
Prof. Mjema amesema
katika utafiti huo ilibainika kuwa asilimia 27 ya walimu wanaofundisha masomo
ya Biashara katika maeneo mbalimbali nchini wana taaluma ya ualimu huku
asilimia 73 wanafundisha kwa kutumia uzoefu jambo linalochangia kupungua kwa ubora wa ufundishaji darasani.
“Sisi kama chuo cha
Elimu ya Biashara tumeona uhitaji uliopo nchini wa kukosa wataalam wa
kufundisha masomo ya Biashara wenye taaaluma ya ualimu ndio maana tumeamua kuanzisha mtaala huu wa kufundishia wanafunzi wa
Shahada ya Elimu katika Biashara ili tupate wahitimu bora watakaofundisha wanafunzi
wetu na kukidhi mahitaji ya soko” Amesisitiza.
Amesema mafunzo
yatakayotolewa yatachukua muda wa miaka 3 na kubainisha kuwa katika mahafali ya
kwanza ya shahada hiyo wanafunzi wapatao 300 wanatarajia kuhitimu mafunzo hayo.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Mafunzo ya awali wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Esther
Mbise akitoa ufafanuzi kuhusu uandaaji wa mtaala huo amesema timu ya wataalam
wa maandalizi ya mtaala huo ilikutana na wadau mbalimbali kutoka Wizara ya
Elimu,Taasisi za elimu, wanafunzi, wazazi na Taasisi za Mitaala ya Elimu ili
kupata maoni yao na kupata maoni yaliyoanisha maeneo ya kufanyia marekebisho
ili kuwa na mtaala bora wenye kukidhi mahitaji ya elimu ya biashara nchini.
Naye Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya mtaala huo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa CBE
akiwasilisha mtaala huo ili upitiwe na wadau wadau waliohudhuria mkutano huo
amesema sababu za kuwepo kwa mabadiliko ya kuwepo kwa mtaala huo ni kuwepo kwa
mahitaji ya wataalam wa kufundisha masomo ya Biashara wenye taaluma ya Ualimu.
Amesema mtaala huo
utakaoanza kutumiwa mwezi Septemba, 2015 utatoa fursa ya wanafunzi wengi zaidi
waliohitimu kidato cha sita na vyuo kujiunga katika masomo hayo ya miaka 3 ya
Shahada ya Elimu katika biashara.
COMMENTS