Simba ilivyoibuka na mabao 2-0 dhidi ya mpinzani wao wa jadi Yanga katika mchezo wa 'Nani mtani Jembe uliochezwa kwenye uwanja wa Tai...
 |
Simba ilivyoibuka na mabao 2-0 dhidi ya mpinzani wao wa jadi Yanga katika mchezo wa 'Nani mtani Jembe uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Awadhi Juma katika dakika ya 30, huku goli la pili likifungwa na Elias Maguli katika dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza. |
 |
Mashabiki wa Simba |
 |
Mchezaji wa Yanga, Haruna Niyonzima akimlaumu mshika kibendera mpira ulipotoka nje na kutoa fursa kwa timu ya Simba kucheza mpira huo. |
 |
Makocha wa Timu ya Yanga, Maxio Maxime (kushoto) na Wa Simba Patrick Phiri wakifuatilia mchezo wa leo. |
 |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenela Mukangara (wa nne kulia), Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamali Malinzi (katikati) pamoja na viongozi wengine wakiwa tayari kwa utoaji wa zawadi. |
 |
Mrisho Ngassa akijaribu kumtoka mpinzani wake Jonasi Mkude bila mafanikio katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. |
 |
Nahodha wa mchezo wa leo, Emanuel Okwi akiwa amenyanyua kombe baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenela Mukangara (kulia). Wa pili (kushoto) ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Jamali Malinzi na viongozi wengine. |
 |
Mlinda mlango wa Simba Ivo Mapunda (kati) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kiwsha kwa mchezo huo na timu yao kuibuka kidedea kwa magoli 2-0. |
 |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenela Mukangaraakisaini mmoja wa mpira ulioshikwa na refa wa mchezo wa leo, Jonesia Rukyaa wakati wa kutoa zawadi kwa washindi na washiriki wa mchezo wa leo. |
 |
Mashabiki wa Yanga wakiwa wamekata tamaa baada ya kufungwa magoli 2-0 katika uwanja wa Taifa Dar leo. |
COMMENTS