Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Angellah Kairuki akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maa...
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Angellah Kairuki akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu
maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya
mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma 3 Oktoba,
2014.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Anna Abdalah akitoa mada wakati wa
mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na
manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma 3 Oktoba, 2014.
Mhadhiri
Msaidizi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Dunford Mpelumbe
akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu
maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya
mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma 3 Oktoba,
2014.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akitoa neno la
shukurani mara baada ya kumalizika kwa utoaji mada kuhusu maandiko ya
kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake
uliofanyika mjini Dodoma 3 Oktoba, 2014.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Sophia Simba akichangia mada wakati wa
mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na
manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma 3 Oktoba, 2014.
Waziri
wa Katiba na Sheria ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
Mhe. Asha-Rose Migiro akichangia mada leo mjini Dodoma kuhusu maandiko
ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya
Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma 3 Oktoba, 2014.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Felister Bura akichangia mada wakati wa
mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na
manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba
inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma 3 Oktoba, 2014.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
04/10/2014.
UMOJA
wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) wamejipongeza kwa hatua kubwa
waliyofikia na manufaa waliyoyapata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya
Katiba inayopendekezwa.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Wabunge hao ambao pia ni Wajumbe wa
Bunge Maalum la Katiba wakati walipofanya semina iliyoandaliwa kwa ajili
ya wajumbe hao kuhusu maandiko ya kisheria na manufaa waliyopata
wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa.
Akitoa
mada wakati wa Semina hiyo, Katibu Mkuu wa TWPG ambaye pia ni Mjumbe wa
bunge hilo, Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa moja ya manufaa ambayo
wanawake watayapata katika Katiba mpya ijayo ni kuhusu masuala ya
uongozi ulio bora wenye kuzingatia sifa na weledi katika michakato ya
ajira na uteuzi ambapo suala hilo limetiliwa nguvu katika Ibara ya 208,
Ibara ndogo ya kwanza kipengele C ambapo katika masuala ya uteuzi na
mambo ya ajira katika nafasi mbalimbali katika Utumishi wa Umma
utazingatia uwezo wa kitaaluma, weledi, ujuzi, usawa wa jinsia hivyo
suala la usawa wa jinsia limezingatiwa.
Mhe.
Kairuki ameongeza kuwa, katika Sura ya Kumi inayohusu masuala ya Bunge
kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 129 ibara ndogo ya Nne, amesema kuwa
kwa kutambua kuwa Bunge ndiyo mhimili muhimu wa dola, Katiba
inayopendekezwa imekusudia kurekebisha kasoro iliyopo ya uwakilishi
mdogo wa wanawake bungeni ambapo hivi sasa kuna asilimia 36.6% ya
wanawake bungeni.
“Kupitia
Katiba hii inayopendekezwa kupitia Ibara ya 129 Ibara ndogo ya Nne
tutakuwa na uwakilishi uliosawa baina ya Wabunge wanawake na Wabunge
wanaume”, alisema Mhe. Kairuki.
Aidha,
alieleza kuwa katika Sura ya 12 inayohusu Mahakama ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama imepewa wajibu katika
ajira mbalimbali na uteuzi kuhakikisha kuwa inazingatia usawa wa
jinsia.
Naye
Mhadhiri Msaidizi wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Dunford
Mpelumbe amewapongeza wajumbe hao wanawake kwa kazi kubwa walioifanya
katika kudai haki zao huku akizungumzia juu ya baadhi ya Mikataba ambayo
Tanzania imeridhia pamoja na baadhi ya itifaki za Kimataifa yakiwemo
maazimio mbalimbali ambayo Tanzania kama Mwanachama wa Jumuiya ya
Kimataifa imeridhia na hatua kubwa iliyopiga.
Mpelumbe amesema kuwa katika Azimio la 1948 (Universal Declaration of Human Rights) katika
Ibara yake ya kwanza inaelezea juu ya mambo ya usawa kati ya mwanamke
na mwanaume, lakini pia suala la usawa kati ya binadamu wote umepewa
kipaumbele.
Mpelumbe
ameongeza kuwa licha ya Mikataba ya Kimataifa pamoja na sheria mama
zilizopo sasa nchini, haki za wanawake zinatakiwa kujengewa ulingo wa
kuzisemea mara kwa mara ili watu wapate kuzielewa vizuri.
“Nchi
za wenzetu wameweka jitihada za dhati kabisa katika kujenga uwezo wa
mwanamke na jitihada hizi zinatokana na utiaji sahihi na kuridhia hii
Mikataba ya Kimataifa mbalimbali ambayo inatoa haki za wanawake lakini
hatua ya pili ni kwa kuchukua hatua za msingi za kikatiba na kisheria
kuziweka hizo haki za mwanamke katika ulingo wa Kimataifa zionekane
zaidi na kwa uwazi kabisa katika Katiba ya nchi na Sheria za nchi”,
alisema Mpelumbe.
Naye
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo, Mhe.
Dkt. Asha-Rose Migiro amesema kuwa mshikamano ambao Wabunge wanawake wa
Bunge hilo wameuonyesha ni mkubwa sana kwani wameweza kushikamana bila
ya kujali Vyama walivyotoka, Kundi waliloliwakilisha , Sura na hata afya
zao.
Dkt.
Migiro ameeleza kuwa suala la hamsini kwa hamsini limekaa vema katika
Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa na itawapa wanawake wengi
msingi wa kuteremka chini kwani wanawake wengi wamejitokeza kwa wingi
katika Mabaraza ya Kata na Taasisi zenye mrengo unaofanana na wamekuwa
waaminifu ndani ya Bunge Maalum.
“Katiba
hii ni yenu, tutakwenda kuipigia debe kwani ni Katiba ambayo imetuweka
mahali pazuri kuimarisha haki ndani ya nchi yetu, maslahi ndani ya taifa
letu, kuimarisha Muungano wetu na umoja wetu”, alisema Dkt. Migiro.
COMMENTS