Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Tigo Mini Kabaang Yaboreshwa Dar es Salaam - ...
![]() |
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tigo Mini Kabaang Yaboreshwa
Dar es Salaam - Septemba 14, 2013. Kampuni ya simu za mkononi Tigo Tanzania leo imetangaza kuboresha kifurushi chake maarufu cha MINI Kabaang ambayo kuanzia sasa itawezesha mteja wa Tigo kupata SMS 450 na kutumia MB 125 ya intaneti na dakika 25 za kupiga simu kwa mtandao wowote ule kwa Tsh 600 tu, badala ya SMS 100, MB 50, dakika 20 kama ilivyokuwa hapo awali.
Kupata huduma ya MINI Kabaang ya SMS 450, MB 125 na dakika 25 za kupiga mtandao wowote wa simu kwa masaa 24 kwa bei ile ile ya Tsh 600 mteja wa Tigo anaweza piga *148*01# na kujisajili katika huduma hiyo.
Akizungumzia maboresho hayo, Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga alisema kwamba huduma hiyo imeboreshwa kwa ajili yakuwafanya wateja wa Tigo kuzidi kutabasamu kwa kuwapatia uwanja mpana zaidi ya kuwasiliana kwa kutuma SMS na kuperuzi katika mtandao wa intaneti.
"Kwa bei ile ile sasa wateja wetu wanapata nyongeza ya dakika 5, SMS 350 na MB 75 za ziada ziliizoongezwa kwenye kifurushi hicho" alisema Mpinga.
Aliongeza, "Tunaamini kwamba maboresho haya yatakidhi kiu ya mawasiliano kwa wateja wetu kote nchini kwa kuwafanya wawasiliane zaidi na kupata taarifa mbali mbali kupitia mtandao wa intaneti.
KUHUSU TIGO:
Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana katika mikoa ishirini na sita (26)
Tanzania bara na visiwani.
Lengo la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya <http://www.millicom.com/> Millicom
International Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko 13 barani
Afrika na Amerika ya Kusini.
COMMENTS