WAREMBO WA SHINDANO LA UTALII LILILOFANYIKA MKOANI TANGA. MISS UTALII TANZANIA KUONGOZA WAREMBO NA WANAMITINDO TANZANIA KATIKAMBI...
WAREMBO WA SHINDANO LA UTALII LILILOFANYIKA MKOANI TANGA. |
MISS
UTALII TANZANIA KUONGOZA WAREMBO NA WANAMITINDO TANZANIA KATIKAMBIO MBIO ZA
NYIKA ZA KUPIGA VITA UJANGILI NA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI
Mshindi
wa Taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Saidi ambaye pia ni Miss
Utalii Morogoro 2012/13, sambamba na washindi wa Taifa na Dunia wa Miss Utalii
Tanzania, wataongoza warembo na washindi wa mashindano yote ya urembo nchini na
nchi jirani, katika mbio za nyika za kimataifa za Ant Poaching International
Marathon, National Parks International Marathon na Wildlife International
Marathon 2013, zitakazo fanyika wakati wa Tamasha la kimataifa la Safari Kuu ya
Utalii Tanzania la "Tanzania Great Safari Tour ' 2013, litakalo fanyika
kuanzia mwezi Agosti hadi Septemba mwaka huu , katika Ukanda wa
Kaskazini,
Kusini, Mashariki na Magharibi wa Utalii.
Mbio
hizo za kimataifa za Nyika za ANT POACHING MARATHON 2013, NATIONAL PARK
MARATHON 2013 na WILDLIFE MARATHON 2013 ni sehemu ya Tamasha la kimataifa la
SAFARI KUU YA KITALII TANZANIA 2013 yaani "TANZANIA GREAT SAFARI TOUR
2013" ambalo pamoja na malengo mengine linalenga katika kuhamasisha vita
dhidi ya Ujangili ikiwemo Uwindaji Haramu, Uvunaji Haramu wa maliasili za
Misitu na Baharini ikiwa ni pamoja na Uvuvi haramu na Uharibifu wa Mazingira. Ujangili
limekuwa ni janga la kitaifa na tishio kubwa la Ustawi na ukuaji wa Utalii
nchini na Duniani, ambapo hatua na juhudi za pamoja zisipochukuliwa sasa basi
wanyama waliopo katika hifadhi za Taifa na Mapori ya akiba watatoweka na
kuziacha hifadhi hizo zikiwa hazina wanyama tena hasa Tembo,Vifaru,Twiga na
jamii nyingi za wanya ambazo hutumika kama kitoweo kwa binadamu.
Upo
ujangili wa uvunaji na usafirishaji haramu wa Misitu ambayo hutoa magogo
na mbao na kuliacha Taifa likipoteza mapato, huku uvunaji huo haramu ukitishia
maeneo ya misitu hiyo kuwa jangwa. Ujangili ukiachiwa utakosesha watoto wetu na
vizazi vijavyo Urithi wa Taifa, lakini pia Taifa litapoteza Mapato yatokanayo
na Utalii na Uvunaji mwingine wa Maliasili za nchi. Ujangili ni uhujumu uchumi,
kwani sekta ya Utalii inachangia zaidi ya 17% ya Pato la Taifa kila mwaka,
zaidi ya 25% ya pato la fedha za kigeni la Taifa na zaidi ya 12% ya ajira zote
nchini na Duniani.
Tamasha
la "Tanzania Great Safari Tour 2013, ni safari kuu ya kitalii, ambayo
itawajumuisha na kuwaweka pamoja waandishi wa Habari, Vyombo vya habari vya
TV, Redio, Magazeti, Majarida, Mitandao ya Intenet, Mitandao ya Kijamii na
Tovuti. Warembo, Wanamitindo, Wanamichezo, Wana Muziki na Wasanii wa Ngoma za
Asili na Filamu, wakitembelea hifadhi za Taifa, Ngorongoro Crater, Mapori ya
Akiba, Hifadhi za Bahari, Maeneo ya Kitamaduni na Kihistoria huku wakipiga
picha za vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vya Televisheni,
Filamu, Video, Minato, Matangazo, Makala, Promo DVD'S, vipindi vya Televisheni
na Majarida wakihamasisha Utalii wa Ndani, vita dhidi ya uwindaji haramu, uvuvi haramu, ujangili na uharibifu wa mazingira, wakitangaza vivutio
vya Utalii Vya Tanzania kitaifa na kimataifa.
Mbali
ya washiriki wa kitaifa, pia kutakuwa na washiriki wa kimataifa,
wanadiplomasia, Viongozi wa serikali, Mashirika ya Kimataifa, Umma, Binafsi na washiriki binafsi ambao wataandikishwa au watakao hamasika kushiriki. Tamasha
la "Tanzania Great Safari Tour 2013 ni tafsiri vitendo ya Sera ya Taifa ya
Utalii, Wanyama Pori, Misitu, Utamaduni ,Uvuvi na Mazingira. Hii itakuwa ni
fulsa nyingine kwa Tanzania na mamlaka zake za Utalii sio kutangaza Vivutio vya
Utalii pekee bali kupiga vita ujangili hususani uwindaji haramu kitaifa na
kimataifa. Aidha hii itakuwa ni fulsa kwa Makampuni, Mashirika, Asasi za Umma
na binafsi kujitangaza kupitia Tamasha hili kwani litarushwa moja kwa moja
(LIVE) katika Televisheni na Internet , na kuangaliwa na zaidi ya watazamaji
680 Milioni Duniani kote. Tamasha hili linaandaliwa na Africa Tourism Promosheni
Centre kwa kushirikiana na Miss Tourism Tanzania Organisation.
COMMENTS