SPIKA JOB NDUGAI AWATAKA VIONGOZI WA DINI NA WATANZANIA KUHUBIRI NA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU NCHINI

Na Benny Mwaipaja, Kondoa SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka watanzania kuwa na uvumilivu wa masuala ya kidini ili nchi ...



Na Benny Mwaipaja, Kondoa
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka watanzania kuwa na uvumilivu wa masuala ya kidini ili nchi iendelee kuwa na amani, utulivu na maendeleo.
Ndugai ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma, alipokuwa akizungumza wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an yaliyowashirikisha zaidi ya watoto na vijana 40 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Spika Ndugai ameeleza kuwa umoja na mshikamano uliopo hapa nchini ni matokeo ya viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini kuendelea kuhubiri amani na utulivu na kuitaka jamii na viongozi hao kuiendeleza kazi hiyo
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameitaka jamii kuendelea kupiga vita uhalifu na kuwafichua wahalifu popote walipo ili nchi iendelee kuwa na amani.
Mratibu na Mwandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'an Tukufu ni kuwajengea vijana maadili mema ili waweze kushiriki kikamilifu kuleta maendeleo ya taifa.
Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Shehe mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Mustapher Shabaan amewapongeza vijana walioshiriki mashindano hayo na kuonesha umahili mkubwa wa kuhifadhi qoran na kuwataka waumini wa kiislamu kusoma na kukielewa kitabu hicho kitukufu kwa kuwa kimejaa elimu na maarifa mengi yatakayo wasaidia kuenenda vyema katika jamii na kupata thawabu kutoka kwa Mungu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), akisisitiza umuhimu wa kuendeleza amani, umoja na mshikamano hapa nchini pamoja na kupinga vitendo vya uhalifu katika jamii, wakati wa mashindano ya ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh N Tashjii, yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma yakiwashirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na kudhaminiwa na Dkt. Ashatu Kijaji, na Benki ya Amana.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, na Mbunge wa Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) akiwa na Mkuu wa Idara ya Masomo wa Benki ya Amana Bi. Rusma Ndoss, wakifuatilia matukio ya mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh n Tashjii, yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma yakiwashirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na kudhaminiwa na Dkt. Ashatu Kijaji, na Benki ya Amana.

Baadhi ya Wabunge na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, wakifuatilia matukio ya mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh N Tashjii, yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma, yakiwashirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na kudhaminiwa na Dkt. Ashatu Kijaji, na Benki ya Amana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Falesy Mohamed Kibassa (mwenye miwani) pamoja na viongozi wengine, wakishuhudia mashindano ya ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh n Tashjii, yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma yakiwashirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na kudhaminiwa na Dkt. Ashatu Kijaji, na Benki ya Amana.

Mmoja wa vijana walioshiriki mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh N Tashjii, akipokea zawadi ya fedha taslimu kutoka meza kuu baada ya kuonesha umahili mkubwa wa kuhifadhi Qur'an kwenye mashindano yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma, yakiwashirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na kudhaminiwa na Dkt. Ashatu Kijaji, na Benki ya Amana.


Meneja wa mashindano ya tatu ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh N Tashjii wilayani Kondoa, ambaye pia ni mume wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, Dkt. Kachwamba, akiwashukuru washiriki na waalikwa wote waliohudhuria mashindano hayo yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma yakiwashirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.



Meza Kuu, wakiongozwa na Mhe. Spika Job Ndugai (wa pili kushoto), wakifuatilia matukio ya mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh N Tashjii, yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma, yakiwashirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na kudhaminiwa na Dkt. Ashatu Kijaji, na Benki ya Amana.


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher Shaaban, akihutubia kabla ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi walioshirikimashindano ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh N Tashjii, yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma, yakiwashirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na kudhaminiwa na Dkt. Ashatu Kijaji, na Benki ya Amana.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa  Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akielezea umuhimu wa vijana kuzingatia elimu ya dini na elimu dunia ili waweze kujenga uzalendo na maadili mema yatakayolisaidia taifa kupiga hatua kimaendeleo, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh N Tashjii, yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, akisisitiza umuhimu wa watanzania kuvumiliana kwenye masuala ya dini, alipopata nafasi ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa  mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya Tajwid, Tahfidh N Tashjii, yaliyofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma yakiwashirikisha zaidi ya vijana 40 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na kudhaminiwa na Dkt. Ashatu Kijaji, na Benki ya Amana. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SPIKA JOB NDUGAI AWATAKA VIONGOZI WA DINI NA WATANZANIA KUHUBIRI NA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU NCHINI
SPIKA JOB NDUGAI AWATAKA VIONGOZI WA DINI NA WATANZANIA KUHUBIRI NA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-pQbtQU9fbP_4HusEwrk69UbL2pQ57APpwAretJGpFbAe0WhA6Esi3XZ6QV0j3zkIG5HehRy3uuyPICP5cxspzoF6-9Bt4HsUJ3gtd-nIUe2AcOQv9k0FNMDKm4kdcBgmGv5xmwqbNcI/s640/AC3A2097.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-pQbtQU9fbP_4HusEwrk69UbL2pQ57APpwAretJGpFbAe0WhA6Esi3XZ6QV0j3zkIG5HehRy3uuyPICP5cxspzoF6-9Bt4HsUJ3gtd-nIUe2AcOQv9k0FNMDKm4kdcBgmGv5xmwqbNcI/s72-c/AC3A2097.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/spika-job-ndugai-awataka-viongozi-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/06/spika-job-ndugai-awataka-viongozi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy