DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO

 MKUU wa wilaya ya Lushoto January Lugangika akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Bumbuli ambacho kwa m...





 MKUU wa wilaya ya Lushoto January Lugangika akizungumza
katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Bumbuli ambacho
kwa mara ya kwanza kilifanyika eneo la makao makuu ya Kwehangara



 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali akizungumza katika
kikao cha robo ya mwaka cha Baraza la Madiwani kilichofanyika eneo Jipya
la Makao Makuu ya Halamshauri hiyo Kwehangala kulia ni Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Amiri Sheiza

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Amiri Sheiza
akizungumza katika kikao hicho kwa kuwataka wananchi kuwa wamoja
kuhakikisha halmashauri hiyo inbapata mafanikio kushoto ni Mkurugenzi
wa Halmashauti ya Bumbuli Peter Nyalali

 Mkurugenzi wa Halmashauti ya Bumbuli Peter Nyalali kushoto
akiwa na Mwenyekiti wa Halma shauri  ya Bumbuli Amiri Sheiza
wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye kikao hicho

 Mkuu wa wilaya ya Lushoto January Lugangika kulia akipitia
makabrasha kwenye kikao hicho

 Sehemu ya madiwani wakifuatilia kikao hicho

 Sehemu ya wananchi waliopata fursa ya kuhudhuria baraza
hilo

MKUU wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga January Lugangika
amewataka madiwani wa halmshauri ya Bumbuli kuhakikisha wanashiriki
katika kukagua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ili
kuiepusha kujengwa chini ya kiwango na hivyo kukosa tija kwa wananchi.
Agizo hilo alilitoa juzi wakati akizungumza kwenye kikao
cha Baraza la Madiwani cha kawaida cha robo tatu kilichofanyika kwa mara
ya kwanza katika makao makuu mapya ya halmashauri hiyo eneo la
Kwehangara.
Alisema iwapo madiwani hao watashindwa kukagua miradi hiyo
inatoa mwanya kwa wakandarasi kushindwa kuitekeleza kwa viwango
vinavyotakiwa hali inayopelekea kukosa tija na thamani halisi ya fedha
zinazotumika.
“Ndugu zangu madiwani hakikisheni mnakagua miradi ya
maendeleo hili ndio jukumu lenu la msingi kwani msipofanya hivyo ndipo
wakandarasi wanafanya miradi hiyo isiwe na tija na hivyo matokeo yake
gharama inayotumika inakosa thamani yake”Alisema DC Lugangika.
Aidha pia alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Peter
Nyalali kuweka utaratibu mzuri kwa madiwani ili waende kukagua miradi
inayotekelezwa hususani miradi ya maji ambayo imekuwa ikihujumiwa
kutokana na wakandarasi”Alisema
Nay kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli
Amiri Sheiza alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwasaidia
kuwatatulia mambo mawili makubwa kwao kuyapatia ufumbuzi.
Alisema suala la kwanza ni ujenzi wa Jengo la Halmashauri
eneo la Kwehangara na pili ni ufunguzi wa kiwanda cha Mponde katika
mambo hayo ameonyesha namna anavyotujali.
“Hivyo tunamuomba Mungu amuongezee hekima na busara katika
kuiendesha nchi na pia napenda kumthibitishia Rais kwamba wananchi,
Baraza la Madiwani pamoja na kupishana kifikra bado tupo pamoja kufanya
kazi bila kubaguana”Alisema.
Hata hivyo alionya kuwa mtu ambaye ataanzisha vimaneno
kuhusu suala hilo watamchukulia hatua kali kwa sababu atakuwa hana nia
njema na wananchi wa halmashauri hiyo katika kuwaletea maendeleo.
“Nionyesha mtu yoyote atakayeleta vimaneno kuhusu suala
hili sisi hatutamvumilia tutamchukulia hatua kali kwani wana Bumbuli na
mbunge wetu sote pamoja “Alisema.
(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO
DC LUSHOTO AWATAKA MADIWANI KUKAGUA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWENYE MAENEO YAO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9i9JTw_bLD3xBBKF6oTdVQzmU0jXojS5xV94g_29oUQT04B0PEsXkPkg0BnZcmT4boaPTjwnlXhG9I2OFoqlslQHOkL_h7BvR29eHcsdjYDO6KdAlbfRYYl9q522-wm371umIGlGh0BQ/s640/_MG_5461.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9i9JTw_bLD3xBBKF6oTdVQzmU0jXojS5xV94g_29oUQT04B0PEsXkPkg0BnZcmT4boaPTjwnlXhG9I2OFoqlslQHOkL_h7BvR29eHcsdjYDO6KdAlbfRYYl9q522-wm371umIGlGh0BQ/s72-c/_MG_5461.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/dc-lushoto-awataka-madiwani-kukagua.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/dc-lushoto-awataka-madiwani-kukagua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy