WAZIRI PROFESA MAKAME MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) KUKAGUA UTENDAJI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiangalia baadhi ya mikataba iliyoingiwa na shirika la Posta Tanzania(TPC)...Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiangalia baadhi ya mikataba iliyoingiwa na shirika la Posta Tanzania(TPC), wakati wa ziara yake kukagua utendaji katika Idara mbalimbali za shirika hilo leo Aprili 17, 2018, jijini Dar es Salaam. Wa pili (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dkt. Haruni Kondo, Wakwanza kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe na Meneja Masoko wa Shirika TPC, David George(Wa tatu kushoto).


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akizungumza na Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati alipofika kwenye Ofisi za shirika hilo, kukagua utendaji katika Idara mbalimbali za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.

Meneja Masoko wa Shirika la Posta, David George akimpatia maelezo Waziri Profesa Mbarawa kuhusu mikataba ya Kibiashara iliyoingiwa na shirika.


Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (katikati), akimweleza jambo Waziri Profesa Mbarawa (kulia), katika ziara hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta, Agnes Mtango. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Usafirishaji ya Shirika la Posta, alipoangalia mfumo wa usafirishaji kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo.

Afisa Msimamizi wa Magari ya Shirika (Transport Officer), Mhandisi Lameck Francis (kulia), akimweleza Waziri Profesa Mbarawa namna ya mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo, unavyofanyakazi.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akikagua mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta ya shirika ya kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo.

Meneja Fedha wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Rajab Mngong'e (kushoto), akimweleza jambo Waziri Profesa Makame Mbarawa, alipofika katika Idara ya Fedha katika ziara hiyo.

Meneja Msaidizi Idara ya Fedha, Aron Samwel (kushoto), akimuonesha Waziri Profesa Makame Mbarawa, mfumo wa utunzaji wa fedha za shirika unavyofanya kazi.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akisindikizwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Elia Madulesi, mara baada ya kumaliza ziara hiyo.


WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Profesa Makame Mbarawa (MB) leo tarehe 17 Aprili, 2018 amefanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.


Mhe. Profesa Mbarawa ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania kwa lengo la kukagua utendaji na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Posta, katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta Luteni Kanali mstaafu Dkt. Haruni Kondo.


Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alitaka kujionea matumizi ya mifumo ya kielektronik na namna ambavyo Shirika limejipanga kuitumia mifumo mbalimbali ili kusimamia utendaji kwa ukaribu.


Mhe. Waziri Mbarawa alitembelea idara ya Fedha, Idara ya Barua na Logistiki, Idara ya Sheria, Idara ya Masoko na pia alikagua mifumo udhibiti wa gharama za mafuta na mwenendo wa magari ya Shirika yanayosafiri kati ya Dar es Salaam na mikoani.


Katika ziara hiyo Mh. Waziri ameitaka menejimenti ya Shirika kusimamia utendaji kazi na kuzingatia weledi na matumizi ya mifumo ya kielektroniki na kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.


Mhe. Waziri alitoa msisitizo wa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi na kukuza tija kwa kila Idara ndani ya Shirka la Posta. Waziri amemwaagiza Kaimu Postamasta Mkuu Hassan Mwang’ombe kufuatilia utendaji wa kila idara na kupata taarifa za mara kwa mara ili kuimarisha utendaji wa shirika.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta alimshukuru Waziri Mhe. Mbarawa kwa kutembelea Shirika la Posta na kuahidi kuwa maagizo yote na maelekezo aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu ili kuleta tija na Ufanisi zaidi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI PROFESA MAKAME MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) KUKAGUA UTENDAJI
WAZIRI PROFESA MAKAME MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) KUKAGUA UTENDAJI
https://4.bp.blogspot.com/-lySHcoF9AFw/WtXyh822swI/AAAAAAACGpU/pc4aJZA6NukqdtduSZ1PM2g8HW_KihNGACLcBGAs/s640/IMG_8898.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-lySHcoF9AFw/WtXyh822swI/AAAAAAACGpU/pc4aJZA6NukqdtduSZ1PM2g8HW_KihNGACLcBGAs/s72-c/IMG_8898.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/waziri-profesa-makame-mbarawa-afanya_17.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/waziri-profesa-makame-mbarawa-afanya_17.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy