MBUNGE RITTA KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA

Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi box la mafuta hayo katibu wa Tas mkoa wa Iringa bwana Leo Sambala katika ukumbi wa halmas...


Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi box la mafuta hayo katibu wa Tas mkoa wa Iringa bwana Leo Sambala katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa  
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi boxi  la mafuta hayo katibu wa Mufindi bwana Andrea Kihwelo
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi  mafuta hayo moja ya walemavu wa ngozi
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi boxi la mafuta hayo mwenyekiti wa wilaya ya Kilolo ndugu Anna Masasi 


Na Fredy Mgunda,Iringa

JAMII imetakiwa kuwalea,
kuwatunza na kuwajali watu wenye ulemavu wa ngozi albino kwa kuhakikisha kwamba
wanaishi katika mazingira mazuri, yenye usalama na sio kuwanyanyapaa pale
wanapohitaji mahitaji yao ya msingi.

Aidha Chama cha walemavu wa
ngozi (TAS) mkoa wa Iringa kimeshauriwa kuendelea kushirikiana na serikali, ili
walemavu hao pia waweze kupata elimu juu ya afya ya usalama wa ngozi pamoja na
kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili katika maisha yao.


Hayo yalisemwa na mbunge wa
viti maalum Ritta Kabati wakati alipokuwa akitoa msaada wa mafuta maalum ya
kupaka watu wenye ulemavu wa ngozi albino katika hafla fupi iliyohudhuriwa na
walemavu hao ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya
Iringa


“Nampongeza
Mwenyekiti wa TAS mkao wa Iringa kwa jitihada zake alizozifanya juu ya namna ya
kupata mafuta haya, kama chama endeleeni kuwa wabunifu namna ya kulisaidia
kundi hili tete la walemavu kwa kuwalea na kuwatunza katika mazingira mazuri”,
alisisitiza mbunge Kabati 

Vilevile Kabati  aliongeza
kwa kuwataka viongozi wa chama hicho kutumia fursa waliyopewa na wanachama wao,
kuhakikisha kwamba wana ainisha matatizo waliyonayo walemavu wa mkoa wa Iringa
na kuyafikisha katika ofisi za serikali ili yaweze kufanyiwa kazi.

Kabati alisema kuwa serikali ya
awamu ya tano inahakikisha kuwa inafakiwa kutatua matatizo ya wananchi wa
ikisha maisha yao yanaboreshwa.

“Hata haya mafuta yamenunuliwa
na serikali kupitia wizara ya afya ,maendeleo ya jamii ,jinsia ,wazee na watoto
na yanasambazwa nchi nzima hivyo sisi viongozi kazi yetu ni kwasaidia usafiri
walememavu hawa” alisema Kabati


Awali akitoa maelezo mafupi juu
ya changamoto zinazowakabili albino katika mkoa wa Iringa huo, Mwenyekiti wao Hellen
Machibya  alisema kuwa wanashindwa
kuwafikia wanachama wake kwa urahisi kutokana na kukosa usafiri na rasilimali
fedha, kwa ajili ya kuwatimizia mahitaji yao ya msingi. 

Machibya alifafanua kuwa
kukosekana kwa fedha kunakwamisha utendaji kazi na uendeshaji wa shughuli
husika, hivyo wanaiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la huruma kwa kutatua
kero zinazowakabili ili kundi hilo tete liweze kusonga mbele kimaendeleo.

Machibya alisema kuwa kazi
aliyoifanya mbunge huyo ni kuokoa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa
kuwa watakuwa wanajikinga na mionzi ya jua.

Machibya alisema kuwa watu
wenye ulemavu wa ngozi wamekuwaathirika wakubwa wa ugonjwa wa kasa kutokana na
ngozi zao kushambuliwa na jua na kusababisha kuiathiri ngozi hivyo msaada
uliotolewa na serikali umeokoa sana maisha.

“Jamani sisi watu wenye ulemavu
tunapenda sana kufanya kazi tatizo mionzi ya jua inatuathiri sana na
kusababisha kushindwa kufanya kazi zetu kwa uwezo wetu hivyo tunaomba serikali
na wadau kama mbunge Ritta Kabati waendelee kutusaidia maana mafuta haya dukani
ni gharama sana hivyo watu wenye ulemavu wa ngozi hatuzimudu” Machibya

Lakini Chama cha walemavu wa
ngozi (TAS) mkoa wa Iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalum Ritta Kabati kwa
kuwasidia kuwafikishia mafuta ya kujipaka mwilini kwa ajili ya kujikinga na
mionzi ya jua ambayo imekuwa ikiwasababishia kupata ugonjwa wa kansa.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MBUNGE RITTA KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA
MBUNGE RITTA KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGKVWRa5IX53idoAKg-iuQknaJnn6O3CpSjsuE2lYETThEEJQGUhftXTdaghXmGJOLyaJytJDM6vxhN5JEyTy8OkJxqk3PPMzRc1bKRzHkCHnLMnLGNEW0AzpKDbTzx3sVq4VDRNGQwhZh/s640/IMG_5000.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGKVWRa5IX53idoAKg-iuQknaJnn6O3CpSjsuE2lYETThEEJQGUhftXTdaghXmGJOLyaJytJDM6vxhN5JEyTy8OkJxqk3PPMzRc1bKRzHkCHnLMnLGNEW0AzpKDbTzx3sVq4VDRNGQwhZh/s72-c/IMG_5000.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/mbunge-ritta-kabati-atoa-msaada-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/01/mbunge-ritta-kabati-atoa-msaada-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy