KAMISHNA SURURU, AKAMILISHA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KWA MAFANIKIO

  Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kulia), akipokea Salamu ya Heshima kutoka kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskaz...



 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kulia), akipokea Salamu ya Heshima kutoka kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Muhsin A. Muhsin akimkaribisha rasmi Kamishna, kutembelea Kituo cha Uhamiaji kilichopo Bandari ya Mkokotoni, Wilaya ya Kaskazini “A” jana tarehe 06 Disemba, 2017 wakati akiendelea na ziara ya kikazi Mkoani Humo. 
 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (juu), akiwaasa watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, kuzingatia Maadili ya kazi, Heshima na Uadilifu kuwa ndio nguzo kwa Utumishi uliotukuka. Pia alikemea vitendo vya Rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu. Alitoa nasha hizo leo tarehe 07 Disemba, 2017 wakati akihitimisha ziara ya siku tatu Mkoani Humo. Kulia kwake ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Muhsin A. Muhsin na kushoto ni Afisa Utumishi, Mrakibu wa Uhamiaji, Ali J. Abdulkadir.

 Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Muhsin A. Muhsin akiwasilisha kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi hiyo kuanzia Julai hadi Novemba, 2017. Huku akitilia mkazo ongezeko la makusanyo ya maduhuli ya Serikali kwa kipindi hicho Dola za Kimarekani 34,000$ zilikusanywa. Alitoa taarifa hiyo leo tarehe 07 Disemba, 2017 wakati Kamishna Sururu akihitimisha ziara ya siku tatu Mkoani Humo. 
 Koplo wa Uhamiaji, Mosi Shadhil Khatib akichangia hoja zilizojadiliwa katika Kikao cha Pamoja cha Wafanyakazi wote wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, Leo tarehe 07 Disemba, 2017 wakati alihitimisha ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani humo. 
 Mkuu wa Bandari ya Mkokotoni, Bwana Ahmed Salim Said, akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zaznibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa aliombatana nao, eneo linalotumiwa na baadhi ya Manahodha kushusha abiria kinyume na utaratibu wa Bandari hiyo, wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye maeneo ya utendaji kazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja jana tarehe 06 Disemba, 2017.
 Sheha wa Shehia ya Mnarani Bwana Mdungi Sharifu Makemi  akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa alioambatana nao, eneo lenye changamoto kubwa wanazokabiliana nazo za Uingiaji wa watu wasiofata sheria katika Ukanda huo.  Alipofanya ziara ya kikazi kwenye maeneo ya utendajikazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja jana tarehe 06 Disemba, 2017
 Sheha wa Shehia ya Nungwi – Banda Kuu Bwana Mohamed Khamis Haji, akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa alioambatana nao, eneo lenye changamoto kubwa wanazokabiliana nazo za Uingiaji wa watu wasiofata sheria katika Ukanda huo.  Alipofanya ziara ya kikazi kwenye maeneo ya utendajikazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja jana tarehe 06 Disemba, 2017
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kulia), akimsikiliza kwa makini Sheha wa Shehia ya Kilindi Bwana Omar Ali Mussa (wa pili kushoto), akitoa shukran zake kwa Uongozi wa Idara kwa ushirikiano mkubwa anaoupata toka kwa Askari wa Uhamiaji. Akisisitiza kauli hiyo Sheha alisema “Ziara yako Kamishna imethibitisha kauli yangu na umeonesha kwa vitendo jinsi ulivyojipanga kushirikiana na wananchi wa eneo letu kutatua changamoto za baadhi wageni wanaoishi hapa bila ya kufata utaratibu” aliyasema hayo jana wakati Kamishna akiendelea na ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMISHNA SURURU, AKAMILISHA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KWA MAFANIKIO
KAMISHNA SURURU, AKAMILISHA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KWA MAFANIKIO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiU0v55-5DjH5TNcg8hepTNdOkaAqypFxqK9vkgd69bd_zNB5QKv1Onn-NRNhH4IQukWlraGGfdlmf0S22TR1WsVy4qrRF8Mnm8gKWRdmo9rEyDN2q6j9yOD8_hlRKa7ncNfeFjfiqyptI/s640/uha1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiU0v55-5DjH5TNcg8hepTNdOkaAqypFxqK9vkgd69bd_zNB5QKv1Onn-NRNhH4IQukWlraGGfdlmf0S22TR1WsVy4qrRF8Mnm8gKWRdmo9rEyDN2q6j9yOD8_hlRKa7ncNfeFjfiqyptI/s72-c/uha1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/kamishna-sururu-akamilisha-ziara-yake.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/kamishna-sururu-akamilisha-ziara-yake.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy