MHANDISI LWENGE ATOA HEKO KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA KUANZISHA MFUMO RAHISI KWA WANANCHI KUPATA TAARIFA ZIHUSUZO NISHATI JADIDIFU

Na Mathias Canal, Lindi Wizara ya Nishati na Madini imetambua kadhia iliyokuwa inawakumba wananchi kupata taarifa sahihi na za uhakika ...



Na Mathias Canal, Lindi


Wizara ya Nishati na Madini imetambua kadhia iliyokuwa inawakumba wananchi kupata taarifa sahihi na za uhakika kuhusu masuala ya nishati jadidifu hapa nchini na hatimaye kuanzisha mfumo rahisishi wa taarifa unaojulikana kama Tanzania Renewable Energy Information Management System (TREIMS).

Mfumno huu utasaidia kuhakikisha kwamba taarifa sahihi za masuala ya nishati jadidifu zinapatikana ambapo pindi taarifa zinapopatikana zitakuwa zinahakikiwa kabla ya kuwafikia watumiaji.




Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge alipowasili kwenye Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge (Mb) amesifu mfumo huo kuwa utapunguza muda wa wadau unaotumika kutafuta taarifa zinazohusu nishati jadidifu sambamba na kufuatilia kwa urahisi maenedeleo ya miradi ya nishati jadidifu inayotekelezwa hapa nchini.

Mhe Lwenge alisema kuwa kulikuwepo na upatikanaji hafifu wa taarifa za masuala ya nishati jadidifu hapa nchini tatizo ambalo lilichangia kuwa na maendeleo kidogo katika sekta ndogo ya nishati jadidifu.

Alisema serikali isingeweza kufikia malengo kwa uduni wa taarifa lakini hatua ambao imefikiwa sasa na Wizara ya nishati na madini itakuwa mbadala wa mafanikio kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mfumo huu unajumuisha taarifa zihusuzo sera, sheria na mifumo mingine ya kisheria inayohusika na usimamizi na uendeleaji wa sekta ndogo ya nishati jadidifu.

Mhandisi Lwenge pia amesifu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvvuvi kwa kurejesha tena Maonesho hayo na Nanenane katika Mkoa wa Lindi ikiwa ni mara ya nne mfululizo huku akieleza kufurahishwa jinsi wananchi wanavyoendelea kujitokeza kupata elimu ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.

Alisema kuwa kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane kwa mwaka 2017 inayosema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” inaakisi mafanikio na fursa kwa kila mwananchi kupata mbinu bora za kilimo mifugo na uvuvi.

Sikukuu ya wakulima inayofahamika kuwa Nanenane ina sherekewa nchini kote tarehe 8 Agosti kila mwaka. Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo. 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MHANDISI LWENGE ATOA HEKO KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA KUANZISHA MFUMO RAHISI KWA WANANCHI KUPATA TAARIFA ZIHUSUZO NISHATI JADIDIFU
MHANDISI LWENGE ATOA HEKO KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA KUANZISHA MFUMO RAHISI KWA WANANCHI KUPATA TAARIFA ZIHUSUZO NISHATI JADIDIFU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgsF-ZJjQfU0UTqSjCaaWir2-XjQct23kSycjfA8RfpmN54BuT3XQ6-E31zPu9wcrTVmTDSt_yf7gzUyiU1Gd2y7oL9FAtQ0S9efXZpbfZ8hw9IHbxuTMwP_E6Hez9feSs8ONfs2LNFIwY/s640/8.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgsF-ZJjQfU0UTqSjCaaWir2-XjQct23kSycjfA8RfpmN54BuT3XQ6-E31zPu9wcrTVmTDSt_yf7gzUyiU1Gd2y7oL9FAtQ0S9efXZpbfZ8hw9IHbxuTMwP_E6Hez9feSs8ONfs2LNFIwY/s72-c/8.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mhandisi-lwenge-atoa-heko-kwa-wizara-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mhandisi-lwenge-atoa-heko-kwa-wizara-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy