DSTV YAZINDUA MSIMU MPYA WA SOKA LIGI YA UINGEREZA KUTANGAZWA KWA KISWAHILI

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akielezea kuhusu msimu mpya wa Soka ndani ya DStv wakati wa hafla maalum ...




Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akielezea kuhusu msimu mpya wa Soka ndani ya DStv wakati wa hafla maalum ya kuzindua kampeni ya msimu wa Soka ijulikanayo kama “Full vyenga Bila Chenga”. Katika hafla hiyo DStv ilitangaza kuwa michezo mingi ya ligi ya Uingereza sasa itakuwa inarushwa kwa lugha ya Kiswahili katika king’amuzi cha DStv. Kulia ni Leyla Patrick na kushoto ni Robert Mgendera wakiwa wamevalia jezi za timu mashuhuri za ligi ya Uingereza


Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akionesha umahiri wake wa kupiga danadana wakati wa baada ya kuongea na wanahabari kuhusu msimu mpya wa Soka ndani ya DStv wakati wa hafla maalum ya kuzindua kampeni ya msimu wa Soka ijulikanayo kama “Full vyenga Bila Chenga”.


DStv yazindua Msimu Mpya wa Soka
Ligi ya Uingereza kutangazwa kwa Kiswahili

Wakati viguvugu la soka ulimwenguni likizidi kupanda, rudimentary Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia king’amuzi cha DStv imezindua kampeni maalum ya Msimu mpya wa Soka ijulikanayo kama ‘Full vyenga Bila Chenga’  ambapo watanzania kupitia DStv wataweza kushuhudia mubashara michuano mikubwa ya soka ulimwenguli inayotarajia kuanza hivi karibuni ikiwemo Ligi kuu ya Uingereza (PL) na ligi ya Hispania (La Liga) pamoja na makombe mengine maarufu Duniani.

Pazia la ligi kuu ya uingereza litafunguliwa jumapili Agosti 6 kwa mtanange wa ngao ya jamii kati ya Arsenal na Chelsea mchezo ambao utaonyeshwa  mubashara kupitia DStv.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande  amesema kuwa msimu huu wa soka, DStv inawahakikishia wateja wake wote kuliona soka katika muonekano bora zaidi huku wakiweza kufuatilia michuano hiyo kwa matangazo yatakayorushwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Msimu huu watanzania, kupitia DStv, siyo tu kwamba wataona michuano mbalimbali ya soka ulimwenguni mubashara, bali pia watayaona katika ubora wa hali ya juu yaani High Definition na zaidi ya yote, tutawapatia fursa watanzania kufuatilia ligi kuu ya Uingereza kwa lugha ya Kiswahili”.

Amesema DStv imeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vipindi na kurekebisha bei za vifurushi ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata fursa ya kujionea matukio mbalimbali muhimu katika Nyanja zote za maisha ikiwemo michezo na burudani. Ametoa mfano wa ligi ya Hispania La Liga ambayo inaonekana yote katika kifurushi cha Bomba. Pia baadhi ya mechi za ligi kuu ya Uingereza (PL) pia zitaonekana katika kifurushi cha Bomba.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria amesema kampeni ya Full Vyenga bila Chenga inamaanisha kuwa wateja wa DStv, msimu huu wa soka wataweza kuliona soka kwa muonekano bora zaidi, yaani bila chenga. “Tunatambua kuwa washabiki wa soka sasa wanataka walione soka vyema, kana kwamba nao wapo uwanjani. Kwa DStv, sasa hata mtu akilambwa chenga utaiona vyema, hata kama mtu anatoka jasho utaliona. Hakuna wingu wala ukungu, ni ‘full vyenga bila chenga’  alisema Alpha.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DSTV YAZINDUA MSIMU MPYA WA SOKA LIGI YA UINGEREZA KUTANGAZWA KWA KISWAHILI
DSTV YAZINDUA MSIMU MPYA WA SOKA LIGI YA UINGEREZA KUTANGAZWA KWA KISWAHILI
https://3.bp.blogspot.com/-xZ4fhrTQm-g/WYQhCDarNmI/AAAAAAAA9zs/wEYl9QTj3XMAkEQLGzvwuO1AvNhUQo84QCLcBGAs/s640/MAHARAGE%2B2.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-xZ4fhrTQm-g/WYQhCDarNmI/AAAAAAAA9zs/wEYl9QTj3XMAkEQLGzvwuO1AvNhUQo84QCLcBGAs/s72-c/MAHARAGE%2B2.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dstv-yazindua-msimu-mpya-wa-soka-ligi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dstv-yazindua-msimu-mpya-wa-soka-ligi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy