F WAZIRI DKT MWAKYEMBE ATOA POLE KWA KITUO CHA RADIO CHA EFM | RobertOkanda

Wednesday, July 12, 2017

WAZIRI DKT MWAKYEMBE ATOA POLE KWA KITUO CHA RADIO CHA EFM


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO

TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe anatoa pole kwa Kituo cha Utangazi cha EFM,familia, ndugu jamaa na marafiki pamoja na Watanzania kwa ujumla kufuatia kifo cha cha aliyekuwa Mtangazaji wa kituo hicho Bw. Seth Katende kilichotokea tarehe 09 /07/2017 katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Waziri Mwakyembe  ametoa pole hizo kufuatia taarifa iliyotolewa na kituo cha Utangazaji cha EFM iliyoeleza kuwa Marehemu Seth  awali alikuwa amelazwa katika Hospitali ya TMJ na baadae kuhamishiwa hospitali ya Taifa Muhimbili mpaka mauti ilipomfika.

Dkt Mwakyembe  amesema kuwa kituo  cha EFM kimepoteza mtangazaji muhimu aliyekuwa anafanya kazi yake kwa umahiri mkubwa hasa katika kipindi chake cha UBAONI.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Imetolewa na:
SIGNATURE-ZAWADI
Zawadi Msalla
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
12/07/2017

0 comments:

Post a Comment