UONGOZI MPYA TAGCO WAKABIDHIWA USUKANI

    Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake, Innocent Mungy, (wa pili kulia), a...

 


 Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake, Innocent Mungy, (wa pili kulia), akimkabidhi nyaraka za chama, Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Abdul Njaidi. ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi majukumu ya kiuongozi jijini Dar es Salaam Julai 20, 2017. Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshughulikia Huduma za Habari na Picha, Rodney Thadeus,
(wa tatu kushoto), Gerald Chami, Mweka Hazina Msaidizi (kushoto) na Peter Malinzi, Mweka Hazina aliyemaliza muda wake.


NA Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.


UONGOZI mpya wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), umekabidhiwa rasmi usukani wa kuongoza taasisi hiyo muhimu katika mawasiloiano ya serikali nchini.


Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam, Julai 20, 2017 ambapo Mwenyekiti wa TAGCO aliyemaliza muda wake, Innocent Mungy, alimkabidhi “nyenzo”
za kufanyia kazi Katibu Mkuu mpya wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi, ambapo shughuli hiyo ilishuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO
anayeshuhulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, Mweka Hazina wa chama  hicho aliyemaliza muda wake,
Peter Malinzi, Mweka Hazina Msaidizi Mteule, Gerald Chami.
Akizungumza  wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekliti aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy alisema, “tunawakabidhi TAGCO, hiki ni chombo muhimu sana kwa mawasiliano ya serikali, hivyo hakikisheni mnakiongoza vyema ili maelengo kusudiwa yafikiwe,”. alisema Mungy.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAGCO, Abdul Njaidi alisema, “Tunashukuru kwa kukabidhiwa
usukani wa TAGCO, tunajua hiki chombo ni muhimu sana katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa taarifa sahihi za shughuli za Serikali yao inazofanya, tutatekeleza majukumu
yetu kwa umakini na uaminifu mkubwa, tunaomba ushirikiano kutoka kwa uongozi uliopita na wanachama wote wa TAGCO na watendaji wote serikalini,”. Alisema Bw. Njaidi
wakati akitoa neon la shukrani.


Viongozi wengine wapya wa TAGCO ni Pascal Shelutete (Mwenyekiti), Sarah Kibonde
Msika (Makamu Mwenyekiti), Tabu Shaibu (Mweka Hazina), Gaudensia Simwanza
(Katibu Msaidizi), Owen Mwandubya (Katibu Mwenezi) na Mpokigwa Mwakasipo (Katibu Mwenezi Msaidizi).

TAGCO ni chama kinachowa kutanisha pamoja Maafisa Mawasiliano wa Taasisi mbambali za umma,
serikali na Halmashauri zote hapa nchini, lengo likiwa ni kupena ujuzi na uwezo wa kuhakikisha taarifa za serikali zinawafikia wananchi kwa usahihi na kwa wakati

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UONGOZI MPYA TAGCO WAKABIDHIWA USUKANI
UONGOZI MPYA TAGCO WAKABIDHIWA USUKANI
https://1.bp.blogspot.com/-aH7rE6TH8c8/WXGVgpRS5RI/AAAAAAAA4j0/euDflPFdWrU3G7n17YeWqlA1oItxSyP9gCLcBGAs/s640/index.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-aH7rE6TH8c8/WXGVgpRS5RI/AAAAAAAA4j0/euDflPFdWrU3G7n17YeWqlA1oItxSyP9gCLcBGAs/s72-c/index.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/uongozi-mpya-tagco-wakabidhiwa-usukani.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/uongozi-mpya-tagco-wakabidhiwa-usukani.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy