TIGO YAKABIDHI DARASA ILILOJENGA KWA SHULE YA MSINGI HACHWI WILAYANI KONDOA

  Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Sezaria Makutta akikata utepe kuashiria kupokea darasa  lenye thamani ya shilingi milioni 8.5  lilil...


 


Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Sezaria Makutta akikata utepe kuashiria kupokea darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 lililojengwa na kampuni ya Tigo kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa, wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata, Mkuu wa kitengo cha usimamizi na mahusiano na serikali kutoka Tigo, Sylvia Balwire na Meneja wa mahusiano na huduma za Jamii kutoka Tigo, Halima Okash (mwenye kilemba) makabidhiano hayo yalifanyika jana. Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Sezaria Makutta akiingia katika  darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 lililojengwa na kampuni ya Tigo kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa, wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata, Mkuu wa kitengo cha usimamizi na mahusiano na serikali kutoka Tigo, Sylvia Balwire na Meneja wa mahusiano na huduma za Jamii kutoka Tigo, Halima Okash(mwenye kilemba).


 
 


Darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 lililojengwa na kampuni ya Tigo kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa, 


Wazazi wakishudia makabidhiano ya darasa lenye thamani ya Milion 8.5 kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa.

Kampuni ya maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania Tigo, Julai 19 2017, imekabidhi darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 kwa shule ya msingi Hachwi iliyoko wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma katika juhudi za kusaidia ukuaji wa kiwango cha elimu wilayani humo.  

Akiongea katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo, Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Kaskazini George Lugata alisema kwamba mchango huo ulikuwa ni sehemu ya juhudi za wafanyakazi wa Kampuni kujitolea na jukumu la kampuni kusaidia maendeleo ya jamii (CSR) katika kusaidia elimu Tanzania.

“Tigo ina sera nzuri ya (CSR) ambayo inasisitiza katika kutoa kwa ajili ya kusaidia Jamii ambako kampuni inaendesha shughuli zake. Tunaamini kwamba kupitia mchango huu, Tigo itakuwa imechangia kwa mara nyingine katika kutengeneza mazingira kwa ajili ya ukuaji wa wataalamu wa baadae kwa ajili ya maendeleo ya haraka ya nchi”, alisema Lugata.  

Katika nafasi yake Meneja wa CSR wa Tigo, Halima Okash, aligusia  vipaumbele vya kampuni vya uwekezaji katika jamii, akisema kwamba Tigo ilikuwa tayari kushirikiana na wadau wengine wenye fikra kama hizo katika juhudi zake za kusaidia maendeleo ya jamii.


Kupitia mpango wetu wa uwekezaji katika jamii, Tigo imekuwa katika mstari wa mbele kuinua sekta ya elimu nchini ambapo tumeshatoa komputa na kuunganisha shule 60 za sekondari kwenye mtandao wa intaneti wenye kasi zaidi kupitia mradi wetu wa e-school pamoja na kuchangia zaidi ya madawati 7,000 kwa shule za msingi nchini kote”alisema Okash. 

 
Mgeni rasmi katika sherehe, Mkuu wa mkoa wa wilaya ya Kondoa, Sezeria Makutta aliishukuru Tigo kwa mchango wake, akibainisha kwamba itasaidia sana katika kupunguza msongamano wa wanafunzi katika darasa moja, ambapo itatengeneza mazingira mazuri ya kujifunzia shuleni.


“Tunawashukuru sana Tigo kwa msaada wao”, alisema Makutta, akiongeza kwamba; “Tunawaomba watu wengine wenye moyo wa kujitolea kujitokeza na kuongeza nguvu katika kuondoa upungufu wa madarasa katika wilaya yetu”.COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIGO YAKABIDHI DARASA ILILOJENGA KWA SHULE YA MSINGI HACHWI WILAYANI KONDOA
TIGO YAKABIDHI DARASA ILILOJENGA KWA SHULE YA MSINGI HACHWI WILAYANI KONDOA
https://4.bp.blogspot.com/-GeOOcK8ffIU/WXGafQkWCPI/AAAAAAAAfFk/hS66cPciaUgxTLIu0_DRlVb595FQLmysACLcBGAs/s640/KUKATA%2BUTEPE.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-GeOOcK8ffIU/WXGafQkWCPI/AAAAAAAAfFk/hS66cPciaUgxTLIu0_DRlVb595FQLmysACLcBGAs/s72-c/KUKATA%2BUTEPE.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/tigo-yakabidhi-darasa-ililojenga-kwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/tigo-yakabidhi-darasa-ililojenga-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy