KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA LITTLE TREASURES SHINYANGA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour ameweka jiwe la Msingi katika shule ya Msingi Little...








Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour ameweka jiwe la Msingi katika shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga.

Amour ameweka jiwe la msingi katika shule hiyo ya Binafsi inayotoa elimu ya awali na msingi leo Jumanne Julai 11,2017.

Akisoma taarifa fupi kwa ki ngozi huyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Kiondo alisema mradi huo wa vyumba vine vya madarasa na matundu nane ya vyoo umegharimu shilingi 120,000,000/=.

“Jengo hili lenye kiwango na ubora wa hali ya juu ili kutoa mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji, lina uwezo wa kubeba wanafunzi 180Madarasa haya manne ni kati ya 15 yaliyopo katika shule hii,ujenzi ulianza mwaka 2016 na umekamilika mwezi Juni 2017 ambapo shule imetumia rasilimali zake za ndani”,alieleza Kiondo.

“Hivi sasa tupo katika mchakato wa kujenga shule ya sekondari ili wahitimu wa shule hii watakaopenda waendelee na masomo ya sekondari hapa hapa,lengo letu ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu kwa mujibu wa matakwa na muongozo wa serikali yetu tukufu”,aliongeza Kiondo.

Naye  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa , Amour Hamad Amour alimpongeza mwekezaji aliyejenga shule hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwekeza katika elimu na kuongeza kuwa serikali inatambua jitihada nzuri zinazofanywa na watu binafsi katika sekta ya elimu nchini.

"Serikali yetu inasisitiza viwanda,ili kufanikisha vizuri zaidi tunahitaji wataalamu wa kuendesha viwanda hivyo,hivyo tunapaswa kuwapa wanafunzi wetu elimu itakayowezesha kupata wasomi waliobobea katika viwanda",alisema Amour.

"Naomba uongozi wa shule ushirikiane na serikali kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na elimu bora inategemea walimu bora,jukumu la uongozi wa shule kuhakikisha kuwa walimu wanaojituma ipasavyo katika ufundishaji",aliongeza Amour.

Angalia picha za matukio yaliyojiri katika shule ya msingi Little Treasures.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour akijiandaa kuweka jiwe la Msingi katika shule ya Msingi Little Treasures leo Jumanne Julai 11,2017.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour akikata utepe wakati wa kuweka jiwe la Msingi katika shule ya Msingi Little Treasures. 


Jiwe la Msingi la Shule ya Msingi Little Treasures limewekwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Amour Hamad Amour.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures,Paul Kiondo akifungua mlango ili kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour Hamad Amour (aliyevaa miwani) aingie ndani ya jengo hilo kuangalia vyumba vya madarasa.Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour Hamad Amour (kushoto) akiwa katika moja ya madarasa ya jengo jipya la shule ya msingi Little Treasures.
Muonekano wa jengo hilo jipya la shule ya msingi Little Treasures lenye vyumba vinne vya madarasa
Jengo jipya la shule ya msingi Little Treasures.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour akizungumza katika shule ya Msingi Little Treasures 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Little Treasures wakimsikiliza kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour akiwa jukwaani na wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures.
Kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akifurahia jambo,anayefuatia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures Paul Kiondo na Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa (wa tatu kushoto akipiga picha wanafunzi wake)
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour akizungumza katika shule ya msingi Little Treasures ambapo alisisitiza wazazi na walezi kusomesha watoto wao kwani elimu ndiyo msingi wa maisha yao.
Kulia ni Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures Paul Kiondo wakifuatilia hotuba ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures.
Wanafunzi wakimsikiliza kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017, Amour Hamad Amour.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiimba wimbo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour (kulia).
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakicheza wimbo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakijiandaa kuushika mwenge wa uhuru.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakishika mwenge wa uhuru
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiendelea kuushika mwenge wa uhuru.Kushoto Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures,Paul Kiondo.
Mwenge wa uhuru ukiondolewa katika shule hiyo.
Gari linalobeba mwenge wa uhuru.Pichani ni baadhi ya wanafunzi wa shule za jirani na shule ya msingi Little Treasures wakiwa eneo la tukio.
Wanafunzi wakiendelea na shughuli zao baada ya mwenge wa uhuru kuondolewa shuleni hapo.
Wanafunzi wakiendelea na masomo.
Jengo la utawala katika shule ya Msingi Little Treasures.
Muonekano wa baadhi ya madarasa katika shule ya msingi Little Treasures. 
Ramani ya Afrika iliyopo shuleni hapo
Majengo yaliyopo katika shule ya msingi Little Treasures.
Magari kwa ajili ya wanafunzi yakiwa shuleni muda wa masomo.

(Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA LITTLE TREASURES SHINYANGA
KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA LITTLE TREASURES SHINYANGA
https://3.bp.blogspot.com/-nOmwNzHJGHk/WWTHGeYhdNI/AAAAAAAAQek/2DPy5uKmo9gRixc_JoiTlFT8o0qthZGZwCLcBGAs/s640/malunde%2B%252824%2529.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-nOmwNzHJGHk/WWTHGeYhdNI/AAAAAAAAQek/2DPy5uKmo9gRixc_JoiTlFT8o0qthZGZwCLcBGAs/s72-c/malunde%2B%252824%2529.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/kiongozi-wa-mbio-za-mwenge-wa-uhuru.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/kiongozi-wa-mbio-za-mwenge-wa-uhuru.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy