Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Salama Aboud Talib akiwahutubia viongozi wapya wa Matawi ya Maji...
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Salama Aboud Talib akiwahutubia viongozi wapya wa Matawi ya Majimbo
ya Chaani na Mkwajuni Kaskazini “A” kichama Unguja.
Katibu wa Idara ya Organazesheni wa
UWT Zanzibar, Tunu Juma Kondo akizungumza na viongozi hao kabla ya
kumkaribisha Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Salama Aboud Talib huko
Gamba Ofisi ya Wilaya Kaskazini “A” Gamba Unguja.
Baadhi ya viongozi mbali mbali UWT wa
ngazi za matawi wa Majimbo ya Chaani na Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini
“A” wakifuatilia kwa makini nasaha zinazotolewa katika Mkutano huo.
Mmoja wa Viongozi wa Tawi la Chaani Mcheza Shauri Bi. Fatma akitoa akizungumza katika Mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu huyo Bi. Salama
Aboud kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Viti Maalum Wilaya ya Kaskazini
“A” Bi. Mtumwa Suleiman sadaka ya fedha kwa Akina Mama wa UWT kwa ajili
ya futari ya Mwezi mtukufu wa ramadhani.
…………………………………………………………………………….
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
UMOJA wa Wanawake wa Chama Cha
Mapinduzi Tanzania (UWT), umewataka viongozi waliochaguliwa kwa ngazi za
matawi ya umoja huo na chama kwa ujumla kuongeza idadi ya wanachama hai
watakaoiwezesha CCM kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.
Wito huo umetolewa na Naibu
Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Bi. Salama Aboud Talib katika ziara ya
kuwapongeza na kuwahamasisha viongozi wapya wa ngazi za matawi
waliochaguliwa hivi karibuni katika Majimbo ya Chaani na Mkwajuni Wilaya
ya Kaskazini “A” kichama Unguja.
Alifafanua kuwa viongozi hao
wanatakiwa kujua idadi kamili ya wanachama na kubaini ni wanachama
wangapi wamefariki ili watolewe katika orodha ya wanachama hai kwa lengo
la kupata idadi ya uhakika ya wanachama watakaoendelea kuibeba CCM
katika michakato mbali mbali ya kisiasa.
Alisema viongozi waliochaguliwa
wameaminiwa hivyo wanatakiwa kuwatumikia na kuwaongoza vizuri
wanachama waliowachagua kwa kutetea maslahi ya CCM kwa vitendo.
Aidha Aliwataka wanawake hao kuwa
na masimamo imara wa kuendelea kuwachagua viongozi wenye sifa na uwezo
wa kuzitumikia chama na jumuiya kwa uadilifu badala ya kuwatumikia watu
wachache wenye nguvu za kisiasa na uwezo wa kifedha.
“Kuweni na msimamo na msikubali
kuyumbishwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi nyinyi chagueni
watu mnaowaamini kuwa watakuongozeni vizuri na kusimamia kwa uadilifu
Chama chetu.
Pia Sote ni binadamu na uongozi
ni jukumu zito lakini naamini kama tutashirikiana kwa kila hatua kazi
zetu zitakuwa rahisi na chama chetu kitaendelea kung’ara na kuongoza
dola”, alisema Bi.Salama.
Hata hivyo kupitia ziara hiyo,
Naibu Katibu Mkuu huyo amesisitiza kudumishwa dhana ya umoja ndani ya
jumuiya hiyo ili wasimamie ipasavyo matakwa ya Katiba ya CCM na Jumuiya
waweze kufanikisha majukumu mbali mbali ya kuendelezwa kwa dhana ya
umoja na mshikamano ndani ya jumuiya hiyo .
Naye Katibu wa CCM wa Wilaya ya
Kaskazini “A” kichama, Ame Omar Mkadam alisema Wilaya hiyo imefanikisha
kwa ufanisi zoezi la uchaguzi kwa ngazi za matawi na kwa sasa
wanaendelea kujipanga na ngazi za Wadi na majimbo ili nazo zifanishe
zoezi hilo kwa ufanisi.
Naye Bi.Fatma Khamis mussa kutoka
Tawi la Chaani, amewasihi viongozi wa ngazi za juu wa umoja huo pamoja
na Chama Cha Mapinduzi kufanya ziara za mara kwa mara katika ngazi za
Matawi ili kuongeza hamasa ushirikiano kwa wanachama na viongozi wa
ngazi hizo.
Pamoja na hayo katika mkutano
huo Naibu Katibu Mkuu huyo Bi. Salama Aboud kwa kushirikiana na
Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Bi. Mtumwa Suleiman
wametoa sadaka ya fedha kwa akina Mama wa UWT kwa ajili ya futari ya
Mwezi mtukufu wa ramadhani.
COMMENTS