RIPOTI YA PILI YA MAKINIKIA: CHENGE, YONA, KARAMAGI, MWANYIKA WAINGIA MATATANI

NA K-VIS BLOG RIPOTI ya pili ya uchunguzi wa mchanga wa madini, (makinikia), iliyokuwa ikiongozwa na mchumi, Profesa Nehemiah Osoro, ...


NA K-VIS BLOG
RIPOTI ya pili ya uchunguzi wa mchanga wa madini, (makinikia), iliyokuwa ikiongozwa na mchumi, Profesa Nehemiah Osoro, imewaweka matatani vigogo kadhaa wa serikali waliostaafu.
Rais John Pombe Magufuli tayari ameagiza viongozi hao ukiondoa marehemu Dkt. Abdallah Kigoda aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, lazima wachunguzwe na hatua za kisheria zichukuliwe.
Kamati imesema kulikuwepo na ukiukwaji mkubwa wa sheria ikiwa ni pamoja na uvunjifu wa sheria uliofanywa na kampuni ya madini ACACIA, na viongozi wa serikali waliopewa dhamana kusimamia sekta ya madini na hivyo kutoa taarifa zisizo sahihi na hivyo kulipotezea taifa zaidi ya shilingi Trilioni 300 katika kipindi chote cha uchimbaji wa madini.
“serikali ifanye uchunguzi wa dhidi ya waliokuwa mawaziri, manaibu mawaziri wanasheria wakuu, makamishna wa madini, wanasheria na makampuni ya upimaji wa madini kwa kuvunja sheria za nchi”. Alisema Profesa Osoro katika mapendekezo ya kamati
Kamati hiyo ya Profesa Osoro imesema tangu mwaka 1998 hadi  Machi 2017, ni makontena zaidi ya 60 na sio 47 kama inavyoonyesha kwenye kumbukumbu za serikali yalisafirishwa nje ya nchi.
Viongozi wastaafu waliotajwa kwenye mapendekezo ya kamati ni pamoja na Mawaziri wa zamani wa Nishati na Madini, Mhe. Daniel Yona, Mhe. Nazir Karamagi, Kamishna wa madini mstaafu Dkt. Dalali Kafumu, Wanasheria wakuu wastaafu, Andrew Chenge na Mwanyika.
Ripoti pia imependekeza kupitiammsajili wa makampuni serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Acacia kwa kuendesha shughuli zake bila usajili.
Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya Wachumi na Wanasheria iliyoundwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, Prof. Nehemia Osoro akiwasilisha Ripoti ya Kamati yake, mbele Rais Magufuli, Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2017.
Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya Wachumi na Wanasheria iliyoundwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, Prof. Nehemia Osoro akiwasilisha Ripoti ya Kamati yake, mbele Rais Magufuli, Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2017

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RIPOTI YA PILI YA MAKINIKIA: CHENGE, YONA, KARAMAGI, MWANYIKA WAINGIA MATATANI
RIPOTI YA PILI YA MAKINIKIA: CHENGE, YONA, KARAMAGI, MWANYIKA WAINGIA MATATANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgoLH7HPEhOOWTGS3AnqBD_alAE6SWQsiUNHPZC-NDnNEfhyphenhyphen90jmFcAJ7zDlZZskFIoIyjp9MOfrLRju3nfFXq_AVGC8wtfCjrMG-Dp8HSgLylnt0oQTvO2TdxTu3g7Vsexpqg9QHJR_A0/s640/jpm.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgoLH7HPEhOOWTGS3AnqBD_alAE6SWQsiUNHPZC-NDnNEfhyphenhyphen90jmFcAJ7zDlZZskFIoIyjp9MOfrLRju3nfFXq_AVGC8wtfCjrMG-Dp8HSgLylnt0oQTvO2TdxTu3g7Vsexpqg9QHJR_A0/s72-c/jpm.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/ripoti-ya-pili-ya-makinikia-chenge-yona.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/ripoti-ya-pili-ya-makinikia-chenge-yona.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy