MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKABIDHIWA VIFAA TIBA VYA UZAZI ZAIDI YA 200 NA BALOZI WA KUWAIT

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akitazama moja ya Dawa,mara baada ya kukabidhiwa mapema leo Ikulu jijini Dar es Salaam. ...Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akitazama moja ya Dawa,mara baada ya kukabidhiwa mapema leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Vifaa tiba vya uzazi zaidi ya 200 na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jasem Al-Najem,vifaa hivyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan vifaa tiba vya uzazi zaidi ya 200 ambavyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Makabidhiano ya vifaa hivyo vya uzazi yamefanyika leo Ikulu ya Dar es Salaam ambapo Balozi wa Kuwait hapa Nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya nchi hiyo imetoa vifaa hivyo kama hatua ya kuendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya nchi hiyo na Tanzania.

Amesema kuwa Serikali ya Kuwait imetoa vifaa hivyo ikiwa ni awamu ya kwanza na lengo ni kutoa vifaa hivyo zaidi ya 1000 vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa wanawake wajawazito na waliojifungua katika hospitali mbalimbali nchini.

Mara baada ya kupokea msaada huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada huo ambao utasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema msaada huo utasaidia sana wanawake wajawazito na waliojifungua kupata vifaa za uzazi ambavyo vinahitajika wakati wanamke mjamzito anapojifungua na baada ya kujifungua.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa vifaa hivyo vitaanza kusambazwa kuanzia mwezi huu na mchakato wa kuainishwa hospitali zitakazopata msaada huo unaendelea.

Makamu wa Rais pia amesisitiza kudumishwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi ya Kuwait na Tanzania kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote Mbili.

Aidha Balozi huyo wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Serakali ya Kuwait itaendelea kusaidia Serikali ya Tanzania katika uimarishaji wa sekta ya afya na elimu nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za msingi

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKABIDHIWA VIFAA TIBA VYA UZAZI ZAIDI YA 200 NA BALOZI WA KUWAIT
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKABIDHIWA VIFAA TIBA VYA UZAZI ZAIDI YA 200 NA BALOZI WA KUWAIT
https://2.bp.blogspot.com/-kmbpvPzrXzk/WUE0ZkwjsdI/AAAAAAADhtk/mdohn1ScUmIqID7DQTFc1akBpZjYD_CrgCLcBGAs/s640/index.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-kmbpvPzrXzk/WUE0ZkwjsdI/AAAAAAADhtk/mdohn1ScUmIqID7DQTFc1akBpZjYD_CrgCLcBGAs/s72-c/index.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/makamu-wa-rais-mhe-samia-suluhu-hassan_17.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/06/makamu-wa-rais-mhe-samia-suluhu-hassan_17.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy