Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa kufungu...
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa
pili kulia) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa kufungua mashindano ya COPA
UMISSETA uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Taifa leo Jijini Dar es
Salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo
wa Wizara hiyo Bw.Yussuph Singo na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa
Rasilimali Watu wa Kampuni ya Coca Cola Eric Ongara na anayefuatia ni
Rais wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) Vitalus Shija.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe
akiongea na wanafunzi wa shule za Sekondari za Jijini Dar es Salaam
wakati wa kufungua kwa mashindano ya COPA UMISSETA katika uwanja wa
mpira wa Taifa.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe
akisalimiana na washiriki wa michezo ya COPA UMISSETA inayoshirikisha
shule za Sekondari za Serikali na Binafsi iliyofunguliwa leo Jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akipiga
mpira kuashiria kufungua mashindano ya michezo ya COPA UMISSETA
inayoshirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi Mei 26 jijini Dar
es Salaam. (Picha na Lorietha Laurence-WHUSM)
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Dhana
ya kuwekeza katika sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa shule za
Sekondari imekua ikileta manufaa makubwa kwa Taifa katika kuzalisha
wachezaji mahiri ambao wamekua wakipeperusha bendera ya Tanzania ndani
na nje ya chini.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe alipokua akifungua michezo ya COPA UMISSETA ambayo
inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi leo katika
Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
“Nimefurahishwa
na juhudi zinazofanywa na Kampuni ya CocaCola katika kuhakikisha
tunaimarisha sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa sekondari kwani kwa
kufanya hivyo tunaibua vipaji na kuviendeleza kwa kupata wanamichezo
mahiri wa baadaye” amesema Waziri Mwakyembe.
Aidha
aliongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa inawekeza katika michezo kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kuwa michezo ni ajira inayowapatia
vijana riziki pamoja na kuchangia katika uchumi wa nchi.
Vilevile
aliwataka walimu kufuata ratiba za vipindi vya michezo kwa kuhamasisha
michezo mashuleni ikiwemo kuwapatia wanafunzi nafasi ya kujifunza na sio
kuvitumia vipindi hivyo kwa shughuli nyingine.
Hata
hivyo Mhe. Mwakyembe aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha kuwa
wanawapatia watoto wao nafasi ya kucheza na kujifunza michezo mbalimbali
inayowajenga kimwili na kiakili.“Michezo inafaida kubwa kwa afya ya
binadamu ikiwemo kuimarisha akili na mwili, kujenga ushirikiano na
urafiki baina ya watu “ alisema Mhe. Mwakyembe.
Naye
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya CocaCola Bw. Eric Ongara
alisema kuwa Kampuni ya CocaCola inaamini katika kuibua vipaji kuanzia
ngazi ya chini ndio maana wamekua wakidhamini mashindano hayo.
Pia
aliongeza kuwa Kampuni ya Coca-Cola itaendelea kushirikiana na Serikali
katika kuhakikisha kuwa michezo inazaa matunda na kufikia lengo
lililokusudiwa la kuibua vipaji vya michezo na kuviendeleza.
Michezo
ya COPA UMISSETA ilifunguliwa rasmi Mjini Dodoma Aprili 28 mwaka huu
ambapo kitaifa yanatarajiwa kuanza Juni 6 hadi 15 mwaka huu katika
Viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza .
COMMENTS