UNESCO KWA KUSHIRIKIANA NA GPF TANZANIA WAENDESHA SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA ,CHUO KIKUU CHA MWALIMU NYERERE

Muandaaji wa Semina hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere  na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza namn...


Muandaaji wa Semina hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere  na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Vijana kutoka Maeneo mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yanazungumziwa wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Kigamboni.
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF), Nelson akieleza namna viongozi katika sekta mbalimbali wanavyoweza kusaidia kudumisha amani katika Jamii.
Mshauri wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi, Anthony Luvanda akitoa
masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea
kwa kufanya shughuli mbalimbali.

 Mwakilishi kutoka Raleigh, Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi
mbalimbali za Kiraia pia alielezea fursa zinazotokana na kujitolea
Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana
jinsi ya kupata 'Scholarship'  zinazotolewa sehemu mbalimbali, na
kuwasihi kuwa wasikate tamaa kwa kuwa kuna nafasi nyingi za kusoma nje ya nchi.
Bwana Charles Ndiku akiwaelekeza vijana namna mbalimbali ambazo zinaweza
kuwasaidia kupata ajira,na aliwasisitiza ili waweze ishi kwa amani
yawapasa kuishi maisha bora ikiwa ni pamoja na kuwa na kipato endelevu.

Mwenyekiti
wa programu kutoka Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
salaam Bw. William Peter akieleza namna vijana wanavyoweza kubadili
mitazamo na kuwa na mawazo chanya ya maendeleo
 Vijana mbalimbali wakichukua yale yaliyokuwa ya Muhimu
 Vijana wakiwa wananyoosha mikono ishara ya kuonesha kuwa wameelewa vizuri kwa yale yote waliyoyasikiliza.

 Vijana wakiwa wanasikiliza kwa Makini.
Semina ikiendelea
Picha ya Pamoja. (Picha na Fredy Njeje)

"Kiongozi bora ni pamoja na yule ambaye anahakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na watu anaowaongoza" hayo yalisemwa na bwana Nelson aliyekuwa
mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Nchini
Tanzania  wakati wa semina ya vijana katika kushiriki programu
mbalimbali za Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana
na Global Peace Foundation Tanzania. 

Alisema kuwa kiongozi makini ni yule anayehakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na kuwafanya wafanyakazi wake waishi kama familia moja ili
kuondoa migogoro mbalimbali ambayo inaweza ikazuirika.

"Amani inatakiwa kudumishwa kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa
ujumla" alisema Nelson na kuongeza kukosekana kwa amani kunaweza
kusababisha  maafa kama vifo kwa sababu ya vita pia uchumi kuyumba
kutokana na watu kuhofia kufanya shughuli za kimaendeleo kwa sababu ya
machafuko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa
uelewa ili wapate kujiunga.
Naye Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili
‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi
zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi
hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.
Mwisho Mshauri na mwezeshaji katika mambo mbalimbali ya Anthony Luvanda aliwasihi vijana kujitambua na kufahamu vipaji vyao na kujua namna ya kutimiza ndoto zao, ambapo aliwaomba pia vijana wasitegemee sana kazi za kuajiliwa bali wawe na mawazo chanya ili kuweza kutimiza malengo yao



Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya vijana 180, kutoka vyuo vikuu vya Mwalimu
Nyerere, CBE, TIA, Bagamoyo, Kampala International University  na St.
Joseph,
wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana wengine



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UNESCO KWA KUSHIRIKIANA NA GPF TANZANIA WAENDESHA SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA ,CHUO KIKUU CHA MWALIMU NYERERE
UNESCO KWA KUSHIRIKIANA NA GPF TANZANIA WAENDESHA SEMINA YA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA ,CHUO KIKUU CHA MWALIMU NYERERE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghmCsJtzfqdhyphenhyphen1YAFG6TxfTPckNsnDycgvUtKIb0P3p0Km78UwtkFh8gcO3d4GCW5YTXR3JW4v23VnT4lvp78xw7Vo1qnAC_t-Pgy7zLDxm0c_AYJ_YMxUr2FuedSxkFe43rOZIF9Tq5o/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghmCsJtzfqdhyphenhyphen1YAFG6TxfTPckNsnDycgvUtKIb0P3p0Km78UwtkFh8gcO3d4GCW5YTXR3JW4v23VnT4lvp78xw7Vo1qnAC_t-Pgy7zLDxm0c_AYJ_YMxUr2FuedSxkFe43rOZIF9Tq5o/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/unesco-kwa-kushirikiana-na-gpf-tanzania.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/unesco-kwa-kushirikiana-na-gpf-tanzania.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy