MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM ATOA CHETI KWA MTUNZA MALI ZA UMMA

Na Leonce Zimbandu MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela ametoa cheti cha shukurani kwa Mkazi wa Mtaa wa Kichangani...






Na Leonce Zimbandu

MKURUGENZI
wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela ametoa cheti cha
shukurani kwa Mkazi wa Mtaa wa Kichangani kata ya Majohe, Gabriel Macheho (pichani) baada ya kutambua mchango wake wakuhifadhi na kutunza rasilimali za umma. 

Moja ya rasilimali hizo ni pamoja na kusimamia eneo
la umma lisichukuliwe na kumilikiwa na watubinafsi, likiwamo eneo
la machimbo ya mchanga lililokuwa likimilikiwa na Mbezi Tile.
Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo,Tabu Shaibu alimkabidhi Macheho cheti hivi karibuni kwa niaba ya Mkurugenzi ili kutoa motisha kwa wananchi wenye moyo wakutoa utetezi wa mali za umma.




Alisema  Manispaa imeamua kutoa cheti hicho baada ya kutambua mchango alio toa mkazi huyo kwa kufuatilia hadi kufanikiwa kupatikana kwa eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii,
ikiwamo ujenzi wa soko na shule.


Tunapaswa kuonesha uzalendo wakufuatilia mambo yenye manufaa kwa jamii ili kuisaidia jamii inayo kuzunguka,”alisema.

Mkazi wa Majohe Andrew Msuya alisema amefurahishwa na kitendo cha
Serikali kutambua mchango wa wananchi wa chini,   hiyo italeta chachu kwa watu wengine kuendeleza na kuhifadhi mazingira.

Naomba serikali kuendelea kuthamini mchango wa watu wa chini kwa kutoa motisha ili kukuza uhusiano mzuri,” alisema.

Gabriel Macheho ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wake
wa kutunza na kuhifadhi rasilimali za umma, kwani wananchi wengi hawakujua kama huo ulikuwa ni wajibu wa msingi kutekeleza.

“Nitaendelea kutoa mchango wangu kwa serikali na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha maeneo ya umma yanaendelea kulindwa na kuhifadhiwa,” alisema.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)




COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM ATOA CHETI KWA MTUNZA MALI ZA UMMA
MKURUGENZI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM ATOA CHETI KWA MTUNZA MALI ZA UMMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYGDRpxh4aUHa3hUkhLWcFNohx64F-ihr71bUfv1NrxOY_U-uuKuiaAi-nQV02dGJp1gDNNfrAhSs7o_ogpX-oSwAzSsZUB7baju8X-BHdjsIA6NQClMG3yaoeWi9rgA-oqelyY-NJzBJU/s320/IMG-20170524-WA0000.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYGDRpxh4aUHa3hUkhLWcFNohx64F-ihr71bUfv1NrxOY_U-uuKuiaAi-nQV02dGJp1gDNNfrAhSs7o_ogpX-oSwAzSsZUB7baju8X-BHdjsIA6NQClMG3yaoeWi9rgA-oqelyY-NJzBJU/s72-c/IMG-20170524-WA0000.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/mkurugenzi-manispaa-ya-ilala-jijini-dar.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/mkurugenzi-manispaa-ya-ilala-jijini-dar.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy