JUMIA TRAVEL YAJIDHATITI KUFANYA MAPINDUZI YA USAFIRI BARANI AFRIKA

Na Jumia Travel Tanzania Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao ndani na nje ya bara la Afrika, Jumia Travel ...


Na Jumia Travel Tanzania

Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao ndani na nje ya bara la Afrika, Jumia Travel imedhamiria kukomboa jitihada za masuala ya usafiri kupitia kampeni yake mpya itakayojulikana kwa ‘DemocratizeTravel.’Akizungumzia juu ya kampeni hiyo Meneja Mkaazi wa Jumia Travel nchini Tanzania, Bi. Fatema Dharsee amebainisha kuwa lengo kubwa ni kuondoa ile dhana potofu kwamba kusafiri ni gharama kubwa na ni jambo gumu ambalo mtu wa kawaida hawezi kulifanya.

“Dhumuni letu kubwa ni kuondoa mawazo yaliyojengeka miongoni mwetu haswa linapokuja suala la mchakato mzima kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hii inamaanisha kupunguza gharama hususani za malazi, upatikanaji wa taarifa pamoja huduma bora kwa kila mtu. Pia kupitia kampeni hii tunataka kuwaonyesha wateja wetu uzuri uliofichika kuhusu bara la Afrika kwa kuwapatia suluhu ya mahitaji yao yote pindi wanapotaka kusafiri kama vile; hatua au mambo ya kuzingatia, malazi, chakula na shughuli za kufanya mahali waendapo,” alisema Bi. Dharsee.


“Hatutoishia hapo bali tunataka pia kuondoa mitazamo tofauti ya kwamba sehemu za kutembelea zilizopo nchi za Magharibi kama vile Ulaya na Marekani au Dubai ni bora zaidi ya Afrika. 


Mbali na kuwarahisishia waafrika kusafiri kwenye maeneo waliyopo lakini pia tunawawezesha kuvuka mipaka kwenda sehemu zingine duniani. Hapa msafiri ataweza kulipia gharama za kusafiri, kwa mfano kwenda jijini London nchini Uingereza, kwa fedha ya nchi yake anayotokea. Hayo yote yanawezekana na yamerahishwa kwani kupitia mtandao wetu mteja ataweza kukata tiketi ya ndege na kufanya huduma ya malazi kwa sehemu anayokwenda kwa wakati mmoja,” aliongezea Meneja Mkaazi wa Jumia Travel nchini.

Kampuni hiyo imesema mbali na kuelekeza kampeni hiyo kwa wateja wake lakini pia itawashirikisha hoteli washirika katika kuhakikisha wanawafikia wateja na kukua kwa haraka zaidi. 

Hayo wanayahakikisha kupitia kuwatangaza mtandaoni ili kukuza muonekana na biashara zao, kuwapatia mifumo ya teknolojia inayoendana na soko la Afrika ili kuwarahishia uendeshaji wa biashara zao kama vile Extranet, SMS au barua pepe pamoja na kuchochea utoaji na uboreshaji wa huduma bora ili kuwavutia wateja wengi zaidi.


“Uzinduzi wa kampeni hii utakwenda sambamba na uwasilishaji wa ripoti yetu ya masuala ya ukarimu na utalii barani Afrika ambayo tutaitoa siku chache zijazo. Kwenye ripoti hii tumezungumzia masuala yote tuliyoyaona kuhusiana na mustakabali mzima wa sekta hii kwa ujumla. 

Lakini pia kutakuwa na shughuli zingine zinaendelea kwenye mitandao ya kijamii kama vile kwa wateja wetu kuwashirikisha wenzao picha au video fupi za sehemu walizotembelea, walijisikiaje na walivutiwa zaidi na vitu gani,” alihitimisha Bi. Dharsee.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: JUMIA TRAVEL YAJIDHATITI KUFANYA MAPINDUZI YA USAFIRI BARANI AFRIKA
JUMIA TRAVEL YAJIDHATITI KUFANYA MAPINDUZI YA USAFIRI BARANI AFRIKA
https://4.bp.blogspot.com/-K41KiGl_abI/WR1gScfk84I/AAAAAAAAarE/gIVcFhdrci8Ee0_DoC1qtStkdvsgJbkCgCLcB/s640/TRAVEL50.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-K41KiGl_abI/WR1gScfk84I/AAAAAAAAarE/gIVcFhdrci8Ee0_DoC1qtStkdvsgJbkCgCLcB/s72-c/TRAVEL50.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/jumia-travel-yajidhatiti-kufanya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/jumia-travel-yajidhatiti-kufanya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy