Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mk...
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza
na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Ruvuma (Hawapo
Pichani) wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Binilith
Mahenge ofisini kwake akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Mahakama
na Kusisitiza Utekelezaji wa Mpango Mkakatiwa Miaka Mitano wa
Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Binilith Mahenge akizungumza.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza
na Watumishi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea (Hawapo Pichani) akiwa
katika ziara ya kukagua shughuli za Mahakama na Kusisitiza Utekelezaji
wa Mpango Mkakatiwa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya
Songea.
Mtendaji
wa Mahakama, Samson Mashalla akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu
Utumishi kwa Watumishi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea (hawapo
pichani) wakati wa ziara ya Jaji Kiongozi kwenye kanda hiyo.
Na Lydia Churi, Songea
Katika
ziara hiyo Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa
Ferdinand Wambali amesema Mahakama itashirikiana na wadau wake ili
kuhakikisha kesi zinamalizika kwa haraka kwenye mahakama mbalimbali
nchini.
Amesema
kupitia nguzo ya tatu ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa mahakama ya
Tanzania ambayo inasisitiza kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama na
ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama, Mahakama itatoa
elimu kwa wananchi pamoja na viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya juu ya
masuala mbalimbali yanayohusu utoaji wa haki kwa wananchi.
Jaji
Kiongozi amesema Mahakama imejiwekea mikakati ya kuhakikisha kesi
zinamalizika kwa wakati na kwa haraka ukiwemo mkakati wa kesi kutokukaa
kwa zaidi ya miaka 2 kwenye Mahakama Kuu, miezi 12 Mahakama za mikoa na
Wilaya pamoja na miezi sita kwenye Mahakam za Mwanzo. Mikakati mingine
ni ile ya kesi kusikilizwa kwa mfululizo na kuwekwa kwa maahirisho
mafupi mafupi ya kesi kwenye Mahakama mbalimbali nchini na Majaji na
Mahakimu kupangiwa idadi ya kesi watazosikiliza katika kipindi cha mwaka
moja.
Aidha, kila Jaji amepangiwa kusikiliza na kumaliza kesi 220 kwa mwaka ambapo Mahakimu wamepangiwa kumaliza kesi 250 kwa mwaka.
Akizungumzia
Maadili kwa watumishi wa Mahakama, Jaji Wambali amewataka watumishi hao
kuwahudumia wananchi wanaofika mahakamani kwa bidii, uaminifu, na
uadilifu ili kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama.
Amesema
watumishi wa Mahakama hawana budi kufanya kazi kwa upendo na
ushirikiano kwa kuwa kazi za mahakama zinategemeana ambapo kila kada ina
umuhimu wake katika wananchi kufikia haki zao za msingi.
Jaji
Kiongozi yuko kwenye ziara katika kanda za Songea na Mtwara kwa ajili
ya kukagua shughuli za kimahakama pamoja na kusisistiza utekelezaji wa
Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania. Tayari
ametembelea mahakama zilizoko Songea mjini na zile za wilaya za Mbinga,
Nyasa, Namtumbo, na Tunduru.
COMMENTS