RC GAMBO AZINDUA BARABARA ARUSHA,AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO, SAMBAMBA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KUSIKILIZA KERO ZAO

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamboa akiwa ameshika mkasi ishara ya kukata utepe katika uzunduzi wa barabara ya St.James na Mahakamani leo...



Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamboa akiwa ameshika mkasi ishara ya kukata utepe katika uzunduzi wa barabara ya St.James na Mahakamani leo Jijini Arusha,Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqarro.Picha na Vero Ignatus Blog.


Watoto wenye ulemavu kutoka shule ya msingi Meru wakiimba wimbo wa Taifa kama picha hapo juu inavyoonekana wakiongozwa na mwalimu Neema Lema ,na hii inayofuata hapa chini wakiongozwa na mtafsiri na mwalimu Viola Wilson .Picha na Vero Ignatus Blog

Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiangalia kwa makini kile ambacho mtoto mwenye ulemavu Amina kutoka shule ya msingi Meru akitumia kompyuta katika kuhariri video aliyoichagua,aliyeshika kipazasauti ni mtaalam wa masomo ya Tehama katika kitengo cha walemavu bi.Betha Denis.Picha na Vero Ignatus Blog.



Na.Vero Ignatus ,Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amtembelea na kujionea mradi wa darasa la watoto wenye ulemavu katika shule ya msingi Meru iliyopo Jijini hapa.


Akiwa katika shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 68 miongoni mwao wasichana wakiwa 34 na wavulana 28 huku walimu viziwi wakiwa wawili na mtaalam mmoja wa kitengo cha I. C. T, Gambo alijionea mwenyewe jinsi wanafunzi hao wanavyofanya kazi kwa kutumia teknolojia hiyo.


Akisoma risala mbele ya Mkuu huyo wa mkoa mwalimu Musa Lwambano alisema shule hiyo unajumla ya walimu 42 ambapo walimu 15 ni wa kitengo na 27 wa shule ya kawaida huku idadi ya wanafunzi ikiwa ni 1,384 wavulana wakiwa ni 709 na wasichana wakiwa ni 675


Amesema shule hiyo inawafadhili kutoka nchi ya Finland walioshirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha lililotoa Sh, milioni 20 na wafadhili wakichangia zaidi ya sh, milioni 180 huku fedha hiyo ikisaidia kujenga jengo bora la ICT na kununua vifaa kama kompyuta mpakato (laptop) 184,deskitopu 5,Projekta 6,Sola 14,Scana Kamera 4,Ipad 22, Mashine ya Laminationi na printa 4.


Pia vijana viziwi wanne wamepata ajira katika kitengo hicho hukuwakimshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kwa kuwawezesha kupata maendeleo hayo shuleni hapo


Gambo alimpongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu na kuwasihi walimu kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wanafunzi hao ili waweze kupata ajira na kujikwamua kiuchumi


Awali Rc Gambo alijionea jinsi wanafunzi hao viziwi wakiimba wimbo wa Taifa kwa kutumia alama zao wakiongozwa na walimu wao ambao ni Veola Wilson na Neema Lema


Gambo anaendelea na ziara yake ya siku tano Jiji hapa kwa kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa barabara ya Mahakama na St, James uliogharimu Sh milioni 586. pamoja na kuzungumza na wananchi ili kutatua kero zao
Gambo amewaagiza watumishi wa jiji la Arusha wakiwemo wataalam wa vitengo mbalimbali kuhakikisha wanatatua kero za wananchi haraka iwezekanavyo ili kuondokana na kero zinazowakabili.

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Visima viwili vya maji vilivyoko magereza vilivyogharimu milioni 372, madarasa 6 Shule ya msingi Olasity,madarasa 4 ya Shule ya msingi Burka Estate ambayo yamegaharimu jumla ya shilingi 218 milioni .

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RC GAMBO AZINDUA BARABARA ARUSHA,AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO, SAMBAMBA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KUSIKILIZA KERO ZAO
RC GAMBO AZINDUA BARABARA ARUSHA,AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO, SAMBAMBA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KUSIKILIZA KERO ZAO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEHIJlOOJThYI5Z7Ir3ZCA6j3gdcAS8aUXY6AoZP5h6EDYg7dZxqTkReE5JPyT-RfhtDxp37WePc6m2lT2wXn6Z8eC1CADl_eS5bYs391qH8x1bc9c2urWnIX4YvJFFDk8yBlC7MIHc3k/s640/IMG_20170426_113307.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEHIJlOOJThYI5Z7Ir3ZCA6j3gdcAS8aUXY6AoZP5h6EDYg7dZxqTkReE5JPyT-RfhtDxp37WePc6m2lT2wXn6Z8eC1CADl_eS5bYs391qH8x1bc9c2urWnIX4YvJFFDk8yBlC7MIHc3k/s72-c/IMG_20170426_113307.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/rc-gambo-azindua-barabara-arushaakagua.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/rc-gambo-azindua-barabara-arushaakagua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy