F JUBILEE NA ZURICH INSURANCE ZAANZISHA BIMA YA AFYA YA GHARAMA NAFUU | RobertOkanda

Thursday, April 20, 2017

JUBILEE NA ZURICH INSURANCE ZAANZISHA BIMA YA AFYA YA GHARAMA NAFUU

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga (katikati), akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Insurance Blockers, Sudi Simba na Rogation Selengia ambaye ni Mkuu wa Uendeshaji wa Idara ya Tiba ya Kampuni ya Jubilee Insurance. Kampuni hizo mbili zitashirikiana kuuendesha mpango huo utakaofadisha familia ya watu wanne kwa kulipa sh. 174,000 kwa mwaka. (PICHA ZOTE NA RICHARD; MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga akizungumza na vyombo vya habari kuhusu manufaa ya bima hiyo wakati akizindua Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.

Mkuu wa Uendeshaji wa Idara ya Tiba ya Kampuni ya Jubilee Insurance, Rogation Selengia akimkabidhi zawadi ya fulana Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Insurance Blockers, Sudi Simba (kushoto) akimkabidhi zawadi ya fulana Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Gharama Nafuu 'Afya Wote'katika hafla iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam. Kampuni hiyo na Jubilee Insurance zitashirikiana kuuendesha mpango huo utakaofadisha familia ya watu wanne kwa kulipa sh. 174,000 kwa mwaka.
Mkuu wa Idara ya Tiba wa Kampuni ya Jubilee Insurance, Keneth Agunda, akielezea kuwa watakaonufaika katika mpango huo ni baba, mama na watoto wawili na endapo familia itataka kuongeza idadi basi kila atakayeongezwa atatozwa sh. 100,000 kwa mwaka.

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Edward Mbanga akifafanua kuwa kwa hivi sasa ni asilimia 25 ya wananchi ndiyo waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hivyo serikali inawakaribisha watu binafsi kuanzisha bima za afya kama kampuni hizo mbili zilivyofanya.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Insurance Blockers, Sudi Simba akiwaelezea wananchi faida mbalimbali watakazopata kupitia bima hiyo ya gharama nafuu.Alitaja huduma zitakazokuwa zinatolewa kuwa ni; magonjwa sugu, huduma za kulazwa, magonjwa ya nje, kulazwa kwa majeraha ya macho-ajali, meno, uzazi wa kujifungua kawaida na upasuaji na ubani wa mazishi kwa kila mwanachama sh. 500,000.


Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi huo.

Baadhi ya maofisa wa kampuni hizo.

Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akiongoza kuimba wimbo wa kampeni ya kuhamasisha kujiunga na bima hiyo.


Akina mama wakitafakari kuhusu mpango huo wa bima

0 comments:

Post a Comment