Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), jana umetiliana saini na kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kut...
Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), jana umetiliana saini na kampuni ya M/S
China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC)
mkataba wa ujenzi wa barabara za Juu ‘Interchange’ katika makutano ya
barabara ya Sam Najoma na Mandela Ubungo jijini Dar es salaam.
Mkataba
huo unamtaka Mkandarasi kampuni ya CCECC kutoka China kuanza ujenzi huo
mara moja na ujenzi huo unatarajiwa kutumia takriban miezi 30 hadi
kukamilika kwake.Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale amesema
zaidi ya shilingi Bilioni 177.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo
utakaowekewa jiwe la msingi mwezi machi mwaka huu.
“Hakikisheni
mnaanza ujenzi mara moja kwani Serikali imeshakamilisha taratibu zote
na tayari kiasi cha shilingi bilioni 2.1 kimelipwa kwa ajili ya fidia
kwa wananchi walioguswa na mradi huo”. Amesema Eng. Mfugale.Ujenzi wa
Ubungo interchange unajengwa kwa fedha ya mkopo kutoka Benki ya Dunia
ambapo Serikali kwa upande wake imeshalipa fidia ya zaidi ya shilingi
bilioni 2.1
“Zaidi
ya magari 65,000 yanapita kila siku katika katika makutano ya barabara
za morogoro,Mandela na sam nujoma eneo la Ubungo hali inayosababisha
msongamano katika barabara ya Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia
jijini Dar es salaam hivyo ufanisi wa mradi huo utahuisha hali ya
usafirishaji katika jiji la Dar es salaam na kuchochea ukuaji wa uchumi”
amesisitiza Eng. Mfugale.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CCECC Bw, Jiang Yigao
amemhakikishia Eng. Mfugale kuwa wataanza maandalizi ya ujenzi huo mara
moja na watafanya kazi hiyo kwa wakati.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale
(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering
Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakibadilisha
hati za mikataba mara baada ya kusaini ujenzi wa barabara za juu eneo
la ubungo (Interchange).
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale
(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering
Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakisaini
mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale
(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering
Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao (Katikati)
wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo
(Interchange).Kushoto ni Meneja Mradi wa ujenzi huo Li Haiquan.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale
akifafanua jambo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa
barabara za juu eneo la ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni
M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China
(CCECC).
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale
akitoa maelezo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara
za juu eneo la ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China
Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Baadhi
ya wawakilishi wa Mkandarasi wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering
Construction Cooperation kutoka China (CCECC) wakifuatilia hafla ya
utiaji saini ya ujenzi wa Ubungo interchange Jijin Dar es salaam.
COMMENTS