TUTAENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO YETU NA BUNGE LA IRAN: NDUGAI

Na Owen Mwandumbya, Bunge Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) amesema Bunge la...



Na Owen Mwandumbya, Bunge

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) amesema Bunge la Tanzania litaendelea kudumisha mahusiano yaliyopo na Bunge Iran ili kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali.

Mhe. Ndugai ameyasema hayo Mjini Dodoma leo alipokutana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika Mheshimiwa ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano wa nchi zetu mbili.

Nashukuru kwa Salaam hizi kutoka kwa Spika wa Bunge la Iran na naahidi kuzifikisha salaam hizi kwa Waheshimiwa Wabunge na pia Ofisi yangu itatolea taarifa juu ya mwaliko huu na kujipanga kutembelea Bunge la Irani kwa kadri muda utakavyoruhusu.  Alisema Mhe. Ndugai

Pamoja na mwaliko huo wa Kibunge kutoka kwa Spika wa Bunge la Iran, Balozi huyo Irani pia alitumia fursa hiyo kuwasilisha ombi la Rais wa Iran Mhe. Hassan Rouhani la kumwalika Mhe. Ndugai ili  aweze pia kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa kusaidia kutatua mgogoro wa muda mrefu kati ya Palestina na Israel uliopangwa   kufanyika tarehe 22 Februari, 2017 Jijini Tehran jambo ambalo pia aliahidi kulitolea majibu hivi karibuni.

Akizungumzia namna ya kuimarisha mahusiano ya Mabunge haya mawili, Mhe. Ndugai alisisitiza umuhimu wa kuanzisha Chama Rafiki cha Kibunge (Parliamentary Friendship Group) baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Iran kwa kuwa kitasaidia sana Wabunge wa Mabunge yote mawili kubadilishana uzoefu na kuimaisha uhusiano uliodumu kwa muda mrefu baina ya Tanzania na Iran.
Kwa upande wa Mhe. Mohammad Dehghani aliipongeza Tanzania kwa kuendelea kuimarisha demokrasia ambayo kwa kiasi kikubwa nchi yake ya Iran imekuwa ikithamini na kuheshimu misingi imara iliyowekwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Nchi yenu imekuwa na historia kubwa sana ya kimahusiano na Iran, pamoja na mambo yote napongeza sana jitihada mnazozichukua kuimarisha demokrasia ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya Wabunge wanawake Bungeni na nimatumaini yetu kuwa mtayafikia malengo mliyojiwekea ya kufikia idadi ya 50 kwa 50. Alisema Bolozi Dehghani

Awali, akimkaribisha mgeni wake, Mhe. Ndugai alimshukuru Mhe. Balozi kwa kutenga muda na kusafiri kutoka Jijini Dar es Salaam kuja Dodoma ambapo pia alitumia nafasi hiyo kumpa pole Mhe. Balozi kwa matukio mawili makubwa yaliyoikumba nchi ya Iran hivi karibuni.

“Mhe. Balozi, kabla ya yote kwa niaba ya Bunge la Tanzania natoa pole kwa msiba mkubwa wa kifo cha Rais wa Nne wa Iran Hayati Akbar Hashemi Rafsanjani kilichotokea taehe 08 Januari, 2017 na pili ni tukio la kuanguka kwa jengo kubwa la kibiashara Jijini Tehran lililosababisha vifo vya watu ishirini (20) na majeruhi zaidi ya 200, tarehe 19 Januari, 2017”. Alisema Mhe. Ndugai

Aidha Mhe. Ndugai alitumia fursa hiyo pia kumshawishi Mhe. Mohammad Dehghani kuanza kufikiria kuhamia Dodoma kwani miundombinu ipo na Ardhi inatosha kabisa kuuwezesha Ubalozi wa Irani kujenga Ofisi na kuendesha shughuli kutokea Dodoma. 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika Mheshimiwa Ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika Mheshimiwa Ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika Mheshimiwa Ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) akipokea mwaliko kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran uliowasilishwa na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili. (Picha na Owen Mwandumbya, Bunge)







COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TUTAENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO YETU NA BUNGE LA IRAN: NDUGAI
TUTAENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO YETU NA BUNGE LA IRAN: NDUGAI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZfKo5vYy5I3qjD-P9wb18QWXv-S9ISqBleWy8D8LgWOF1kr89jRQEzWlRQfRfgC9zX0WAP9ieDMO33WVyZ1bo6MfLRVvVSF-5ZqRA-R6NgXOFW1pHSB56zruRkUhVyfe20d7p-fm4pOI/s640/Pic+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZfKo5vYy5I3qjD-P9wb18QWXv-S9ISqBleWy8D8LgWOF1kr89jRQEzWlRQfRfgC9zX0WAP9ieDMO33WVyZ1bo6MfLRVvVSF-5ZqRA-R6NgXOFW1pHSB56zruRkUhVyfe20d7p-fm4pOI/s72-c/Pic+1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/tutaendelea-kuimarisha-mahusiano-yetu.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/tutaendelea-kuimarisha-mahusiano-yetu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy