PSPF YAWAPIGA MSASA WATUMISHI OFISI YA RAS DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akipeana mikono na Katibu Tawala Msaidizi (anayeshughulikia masual...









Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akipeana mikono na Katibu Tawala Msaidizi (anayeshughulikia masuala ya serikali za mitaa),
jijini Dar es Salaam, Merry Assey, baada ya kufungua semina ya mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam, iliyoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika Januari 3, 2017 kwenye makao makuu ya PSPF Golden Jubilee
Towers jijini.






NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umeendesha semina ya mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, ili kuwajengea uwezo wa kushughulikia matatizo ya
wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo.
Mafunzo hayo ya siku mbili, yameanza leo Januari 3, 2017, na kufunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi (sehemu ya serikali za mitaa), Bi. Merry Assey kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ea Dar es Salaam, Paul Makonda.
“Niipongeze PSPF kwa kuandaa semina hii ambayo inatoa fursa ya watumishi hawa waliohudhuria katika mafunzo haya kuelewa huduma na shughuli zinazofanywa na Mfuko huu na kwa
maana hiyo iwe rahisi kwenu kutatua kero za wananchi wanaofika pale Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kutafuta ufumbuzi hususan kwa wanachama wa Mfuko huu,.” Alisema
Bi. Assey, wakati akifungua semina hiyo.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, alisema, PSPF ilifikia
uamuzi wa kuandaa semina hiyo kufuatia wazo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye alitaka kujengewa uwezo kwa watumishi wa Ofisi yake ili waweze kuwahudumia vema wananchi wakiwemo wanachama wa PSPF.
“Nililipokea wazo hilo na sisi PSPF tukaona ni fursa nzuri kwa kuwaelimisha watumishi hawa ambao, ninahakika baada ya mafunzo haya, watakuwa mabalozi wetu wazuri lakini pia
na wao watajiunga na Mfuko huu.” Alisema Bw. Mayingu.
Mada mbalimbali zilitolewa kwa wanasemina hao ikiwa ni pamoja na ile ya shughuli za
Mfuko iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma wa Mfuko huo, Bi. Neema Muro, Kaimu Meneja Mafao, Bw. Haji Moshi na Maafisa wengine wa Mfujko huo.


 Bi. Merry Assey, akifungua semina hiyo.

 Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia kwa makini.

 Meneja Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi. Costantina Martin, akizungumza wakati wa semina hiyo.

 Mkurugenzi wa Huduma wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi. Neema Muro akitoa mada juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko wa Pensehni wa PSPF.

 Kaimu Meneja Mafao wa PSPF, Bw. Haji Moshi, akitoa mada ya namna mwanachama wa Mfuko huo anavyoweza kupata mafao yake.
 Bw. Haji Moshi akitoa mada.

 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitoelwa na viongozi na maafisa wa PSPF.

Baadhi ya washiriki wakipitia vijarida vyenye maelezo ya kina kuhusu huduma zitolewazo na PSPF.

 Mshiriki akisoma kijarida cha PSPF.

 Mkurugenzi wa Huduma wa PSPF, Bi. Neema Muro, (wapili kulia), akiongozana na Mameneja na maafisa wa Mfuko huo wakati wakielekea chumba cha semina kutoa mafunzo kuhusu huduma za Mfuko.

 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.

  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa PSPF na Ofisi ya RAS, Dar es Salaam.

 Picha ya pamoja.
Baadhi ya mameneja wa PSPF wakiwa katika picha ya pamoja na "meza kuu"

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PSPF YAWAPIGA MSASA WATUMISHI OFISI YA RAS DAR ES SALAAM
PSPF YAWAPIGA MSASA WATUMISHI OFISI YA RAS DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhMDOwRTuRMVvUQR1oak84RCMcHViPq2r166_rzvzaswzj7g7k87s94NZ9jiELvvdPVsP9NjZf11K2Nk1z6gbGX-qx4sQNRtoY_T-rlAtsUpKeeBdUem3lcOJlbtMbhxaa0Beq-9icyS4/s640/DG_PSPF.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhMDOwRTuRMVvUQR1oak84RCMcHViPq2r166_rzvzaswzj7g7k87s94NZ9jiELvvdPVsP9NjZf11K2Nk1z6gbGX-qx4sQNRtoY_T-rlAtsUpKeeBdUem3lcOJlbtMbhxaa0Beq-9icyS4/s72-c/DG_PSPF.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/pspf-yawapiga-msasa-watumishi-ofisi-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/pspf-yawapiga-msasa-watumishi-ofisi-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy