Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Mmiliki mwenza wa kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi amefikishwa katika mahakama ya haki...
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mmiliki
mwenza wa kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi amefikishwa katika
mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kuunganishwa katika mashtaka yaleyale
yanayomkabili mkurugenzi wa kampuni hiyo, Maxence Melo.
Washtakiwa wote wawili walisomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na Hakimu mkazi mkuu, Godfrey Mwambapa.
Wakili
wa serikali, Mohamed Salum alisema kuwa washtakiwa hao wakiwa eneo la
mikocheni kwa nafasi zao wakijua jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa
mawasiliano kwa njia ya mtandao kufuatia chapisho lililochapishwa katika
tovuti yao na waliamua kushindwakutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi kwa kuwanyima data walizonazo.
Hata
hivyo upelelezi wa kesi hizo mbili umekamilika na washtakiwa wote hawa
watasomewa mashataka yao kuanzia Februari 9 na Februari 20.
Mpaka
sasa washtakiwa wote wawili wapo nje kwa dhamana kwa masharti ya bondi
ya Milioni 10 kwa kila kosa na masharti ya kutosafiri nje ya nchi.
Maxence Melo akijaribu kumueleza jambo mmiliki mwenza wa Jamii Forum Mike mushi ndani ya chumba cha Mahakama
Maxence Melo na Mike Mushi wakimsikiliza wakili wao
COMMENTS