KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, MPINGO HOUSE

Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii (WMU) Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imetembelea makao makuu ya Wizara ya ...


Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii (WMU)
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imetembelea makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House jijini Dar es Salaam leo na kuzuru ghala la nyara za Serikali kuona utunzaji wa meno ya tembo na changamoto zake.
Kabla ya kutembelea ghala hilo kamati hiyo ilipokea taarifa maalum ya wizara juu ya mchakato mzima wa taratibu za ukusanyaji wa meno ya tembo, usafirishaji, uhakiki, usajili kwenye mfumo maalum wa kielektroniki, uhifadhi wake na ulinzi thabiti wa ghara hilo.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Idara ya Wanyamapori, Bw. Robert Mande alisema meno yanayohifadhiwa katika ghala hilo ni yale yanayotokana na vifo asilia, kuuawa kutokana na uharibifu wa mali na maisha ya binadamu na yale yanayotokana na ujangili.
Waziri wa Maliasili na utalii, Prof. Jumanne Maghembe akijibu moja ya swali la wajumbe wa kamati hiyo ambao walitaka kujua uwezekano wa kuuza meno hayo ya tembo yaliyohifadhiwa ili kulipatia taifa mapato,  amesema msimamo wa Serikali ya Tanzania kwa sasa sio wa kuuza wala wa kuchoma meno hayo.
"Msimamo wetu ni kama ule wa nchi za Kenya, Uganda, Zambia, Malawi na Msumbiji wa kutokuuza meno haya kwa sasa kwasababu mbalimbali za kimsingi kabisa, moja ikiwa ni sababu za kiutafiti ambapo vinasaba vya meno ya zamani vinaweza kutumika kubaini mambo mbalimbali ikiwemo utafutaji wa dawa ya magonjwa ya tembo”, alisema Maghembe.
Alisema kitendo cha kuuza meno hayo pia ni kuchochea zaidi biashara hiyo kwakuwa kitaongeza upatikanaji wa bidhaa hiyo kwenye masoko hivyo kuendelea kuipa uhai biashara hiyo haramu duniani.
Hapo awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Generali, Gaudence Milanzi akizungumza kwenye kikao cha kamati hiyo mkoani morogoro kilichohusisha uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) alisema ujangili hapa nchini kwa sasa umepungua kwa kiasi kikubwa na kwamba nyara zinazokamatwa kwa sasa ikiwemo meno ya tembo ni za zamani zilizokuwa zikisubiria kusafirishwa nje ya nchi.
Alisema hatua hiyo ya kupungua kwa uhalifu huo imefanikiwa kutokana na kazi kubwa inayofanywa vikosi maalum vya Askari wa wanyamapori vya kudhibiti ujangili kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini.
Alisema hatua ya Serikali ya China kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo nchini humo ni jambo la kupongezwa na kwamba uamuzi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msukumo wa vitendo vya ujangili nchini na barani Afrika kwa ujumla.
Naye mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Nditiye amewapongeza viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii namna walivyojipanga katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo na kuwaahidi ushirikiano kutoka kwa kamati yake.
Aliahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi wa wizara hiyo katika kuhakikisha kuwa wanaikabili changamoto kubwa ya uvamizi wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi. "Sisi tunaungana na nyie, hatukubali mifugo kwenye hifadhi zetu, kwakuwa zinaharibu ubora wa hifadhi hizo, tunawaahidi ushirikiano wa kukabiliana ma changamoto hiyo"
Kamati hiyo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilitembela pia makao makuu ya Wakala ya Mbegu za Miti Tanzania (TTSA), Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) zote za mkoani Morogoro.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizaya hiyo, Meja Generali Gaudence Milanzi (kushoto) wakiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipowasili katika ofisi za Wakala ya Mbegu za Miti Tanzania (TTSA) mjini Morogoro jana kwa ajili ya kuona kazi na miradi ya wakala huyo. Kushoto ni wajumbe wa kamati hiyo, Silafi Maufi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa na Godwin Molel (wa pili kushoto), Mbunge wa jimbo la Siha. (Picha na Hamza Temba - WMU)

Mtaalam wa Baiolojia ya mbegu wa Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania, Fandey Mashimba (kulia) akitoa ufafanuzi wa namna ya uaandaaji wa mbegu na miche ya miti kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea wakala huyo jana Mkoani Morogoro kwa ajili ya kuona shughuli na miradi ya wakala huyo. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.

Meneja wa Kanda ya Mashariki na Kati wa Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania, Frida Mngulwi (kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii namna mashine za kuandaa mbegu za miti zinavyofanya kazi walipotembelea ofisi za Wakala huyo jana mkoani Morogoro. Wa pili kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA), Edigar Masunga (mbele kushoto) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kukaga shamba la miti la wakala huyo mkoani Morogoro jana.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisistiza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) mkoani Morogoro jana.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utali, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa wakati kamati ya bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA ) na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) mkoani Morogoro jana






COMMENTS

BLOGGER: 1
Loading...
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, MPINGO HOUSE
KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, MPINGO HOUSE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjINea5qsiCuIZCF5K5ouNxj0DJLiHb5p5R7cXd7npit_KTDhJMOblkmgmG8eHaVpNRr0sdrSR-R2cRSV4v8Wd6oOGN24EtiN_gadRmY5wfdbI8y7f-vOrWx9Cp_10jw1N1dbTeefoaTHQ/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjINea5qsiCuIZCF5K5ouNxj0DJLiHb5p5R7cXd7npit_KTDhJMOblkmgmG8eHaVpNRr0sdrSR-R2cRSV4v8Wd6oOGN24EtiN_gadRmY5wfdbI8y7f-vOrWx9Cp_10jw1N1dbTeefoaTHQ/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/kamati-ya-bunge-ya-ardhi-maliasili-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/kamati-ya-bunge-ya-ardhi-maliasili-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy